Ticker

10/recent/ticker-posts

Dun&Bradstreet wazindua alama ya mkopo kurahisisha utoaji wa mikopo nchini

Taasisi inayoongoza kuandaa taarifa za mikopo nchini Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Ltd. imezindua mfumo wa alama ya kwanza ya utabiri wa deni la mteja ili kuwawezesha wakopeshaji kama vile benki na taasisi za huduma ndogo za fedha kupata taarifa sahihi za wakopaji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu Mtendaji wa Dun & Bradstreet Credit Bureau, Miguel Llenas alisema kuwa alama hiyo imezinduliwa ili kutatua changamoto zinazowakabili wadau wote katika soko la mikopo nchini.

Alisema mfumo wa alama hiyo utaongeza uwajibikaji katika kukopesha na kukopa, pia utasaidia wakopeshaji na wadai kusimamia vitabu vyao vya mkopo na kuhakikisha viwango vya riba hulingana na maelezo husika ya mkopaji na kukuza bidhaa za mkopo katika soko la wakopeshaji.

Alisema Alama ya Mikopo hutoa faida nyingi kwa mkopaji kwani humwezesha kujua kama anavyo vigezo vya kukopa au kutokukopa.

“Pia inapunguza muda wa kupata mkopo kulingana na taarifa za mkopo zilizopo kwenye ripoti zake hivyo kukuwezesha kama dhamana ya mkopo wako mpya na kukupatia mkataba bora na wenye kiwango stahiki cha riba.

"Inampa mkopeshaji taarifa sahihi za mchakato wa utoaji wa mikopo; ujumbe na mwongozo wa tathmini ya mkopaji, pia kuwezesha kasi ya utoaji mkopo na usimamizi wa wateja husika. "Pia mtoaji wa huduma anaweza kuongeza kasi ya upatikanaji wa wateja, kuelekeza na kusimamia mipaka ya mkopo yao na kuboresha utoaji wa huduma hizo.

Akifafanua zaidi kuhusu huduma hizo, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Adebowale Atobatele alisema lengo lao kila wakati limekuwa kutoa suluhisho la usimamizi kuelekea mikopo isiyolipika katika sekta mbalimbali na kutoa taarifa sahihi kwa watoa mikopo kufanya maamuzi sahihi ya kutoa au kutokutoa mikopo.

"Lakini pia kuharakisha kasi yao ya kuchukua maamuzi; kurahisishaji upatikanaji wa haraka wa bidhaa za mikopo kwa kampuni zinazostahiki, watu binafsi na hivyo kukuza fursa za ukuaji kwa uchumi kwa wote.

“Pia tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wote na wahusika wote nchini ili kusaidia kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za mkopo nchini, "alisema. Alisema alama ya mkopo ni maelezo ya kihesabu ambayo wakopeshaji hutumia, pamoja na ripoti ya mkopo kutathmini hatari ya kutoa mkopo.

"Alama za mkopo ni njia muhimu za kukopesha ambayo inaweza kuamua ikiwa unapata mkopo, viwango gani vya riba unalipa kwa deni husika, "alisema.

Naye Ofisa Mkuu wa masuala ya Ufundi wa kampuni hiyo, Kelyn Pena alisema alama ya mkopo ya watumiaji wa D & B ni ya kipekee nchini Tanzania kwa sababu inatoa taarifa halisi za kitakwimu. "Alama hii ya mkopo ni rahisi kutumiwa na taasisi za kifedha na watumiaji kwa jumla kwani iko thabiti katika mpangilio wa wakati na utofauti wa historia ya mikopo ya watumiaji. " alisema.


Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa fedha kutoka BOT, Jerry Sabi akizungumza namna mfumo wa alama za mkopo kwa wakopaji na wakopeshaji unavyosaidia kukuza sekta ya fedha na uchumi nchini.


Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Dun&Bradstreet Credit Bureau, Miguel Llenas akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mfumo wa alama ya mkopo kwa wakopaji na wakopeshaji nchini. Mfumo huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam kuwawezesha wakopeshaji kuwa na taarifa sahihi za wakopaji.

Meneja Mkuu wa kampuni ya Dun&Bradstreet Credit Bureau, Adebowale Atobatele akifafanua namna mfumo wa alama kwa mteja unavyozisaidia taasisi zinazokopesha wateja kupata taarifa sahihi za mkopaji.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NbVixA
via

Post a Comment

0 Comments