DIT YATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU

  Masama Blog      
TAASISI ya Teknolojia ya Dar es Dar es Salaam (DIT) kuanzia 21 hadi 25 Oktoba 2019 inaendesha mafunzo ya TEHAMA ya siku tano kwa walimu wa shule za serikali nchini. 
 Lengo la mafunzo hayo ambayo yanajulikana kitaalamu 'Basic ICT Devices Maintenance and Repair' ni kuimarisha utunzaji wa vifaa vya TEHAMA ambavyo hutolewa kwa shule mbalinbali nchini na serikali pamoja na wadau wengine, vifaa hivyo ni ambavyo ni pamoja na kompyuta, printa na vifaa vya mawasiliano. 
 Mafunzo hayo yanayotolewa na wataalamu wa DIT yamefadhiliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (UCSAF). 
Walimu wanaohudhulia mafunzo hayo ni wa shule za Msingi na Sekondari. 
“Serikali hutoa vifaa mashuleni kama kompyuta, printa au vifaa vya mawasiliano kupitia UCSAF, imeonekana kuwa ni muhimu vifaa hivyo vikatunzwa vizuri hivyo tutoe mafunzo kwa walimu hawa ili waweze kutunza na kufanya ukarabati.
“Walimu tuliowapokea hapa ni 540 na mafunzo haya yanaanza leo Jumatatu na yatafungwa Ijumaa, ni mafunzo ya siku tano,” alisema Mratibu wa Mafunzo kutoka DIT, Daudi Mboma. 
Walimu hao ni kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Pwani, Mtwara, Ruvuma, Lindi, Kilimanjaro, Kilimajaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Zanzibar na Tanga. Mwisho


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33SAQsj
via
logoblog

Thanks for reading DIT YATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU

Previous
« Prev Post