DC KINONDONI AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUSHUHUDIA RC MAKONDA AKIZINDUA UJENZI WA BARABARA YA MAKONGO JIJINI DAR

  Masama Blog      
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KERO ya barabara Makongo jijini Dar es Salaam inatarajia kufika ukingoni baada ya Serikali ya Rais Dk.John Magufuli kutoa Sh.bilioni 8.9 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa kipande cha kilometa tano ambazo zilizokuwa zimebakia ili kuunganisha maeneo ya Goba, Mbezi Massana, Mbezi mwisho na Wazo kwa lami.

Akizungumza leo na wananchi wa Kilimahewa Juu na Salasala katika Kata ya Wazo wilayani kinondoni, Mkuu wa wilaya hiyo Daniel Chongolo amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anatarajiwa kuzindua ujenzi wa barabara hiyo Ijumaa ya wiki hii.

Chongolo amefafanua kuwa wananchi wa Makongo walikuwa wakifanyiwa kila aina ya utani na wenzao wa maeneo yenye miundombinu mizuri ya barabara ikiwa ni pamoja na kuwachora kwenye vibonzo kuwa ni watu wanaofika mjini wakiwa wamechafuka vumbi kila mahali, lakin sasa muda mfupi ujao hali hiyo itakoma na wao wataanza kutereza kama wengine.

Ameongeza kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo ya Makongo ni sehemu ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya barabara unaoendelea ndani ya Wilaya ya Kinondoni huku akitumia nafasi hiyo kueleza  Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kutatua kero za wananchi wakiwamo wa wilaya hiyo. "Miradi mingine ya barabara ni pamoja na ule wa Ununio kwenda Mbweni ambako ujenzi wake unaendelea kwa awamu, umaliziaji wa kipande cha barabara ya Wazo kiwandani mpaka Kisauke shule kata ya Wazo.

"Pia upanuzi wa barabara ya Morocco kwenda Mwenge, upanuzi wa barabara ya Shekilango kwa njia nne, na uboreshaji wa barabara zaidi ya 46 za mitaa kwenye maeneo ya Tandale, Mburahati, Ndugumbi, Mwananyamala, Makumbusho, Kijitonyama na Magomeni,"amesema.

Chongolo ametoa mwito kwa wananchi wa Makongo na maeneo yanayozunguka eneo hilo kujitokeza kwa wingi katika shughuli hiyo ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo muhimu ya Makongo siku ha ijumaa."Wananchi tunaomba mjitokeze kwa wingi siku ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo.

Hata hivyo wakati anaeleza uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo, wananchi wa Kilimahewa na Salasala wamemuhakikishia Mkuu wa wilaya hiyo kwamba watajitokeza kwa wingi ili nao kuwa sehemu ya kushuhudia kazi ambayo itafanyika katika kuijenga barabara hiyo ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu. 
Mkuu wa Wilya ya Kinondoni ,Daniel Chongolo akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Kilimahewa Juu,kata ya Wazo wilayani Kinondoni changamoto zake,mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa eneo alipofanya ziara fupi ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo ya barabara na maji,lakini pia aliwaeleza tukio la uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Makongo unaotarajiwa kufanywa na Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda Ijumaa wiki hii.
  Wananchi wa Kilimahewa Juu katika Kata ya Wazo wilayani kinondoni, wakimsikiliza Mkuu wa wilaya hiyo Daniel Chongolo amesema kuwa Mkuu alipokuwa akizungumza na wakazi hao kuhusu uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Makongo unaotarajiwa kufanywa na Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda Ijumaa wiki hii.DC Chongolo aliongeza kusema kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo ya Makongo ni sehemu ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya barabara unaoendelea ndani ya Wilaya ya Kinondoni huku akitumia nafasi hiyo kueleza  Serikali ya Awamu ya Tano kudhamiria kwa dhati kutatua kero za wananchi wakiwamo wa wilaya hiyo. "Miradi mingine ya barabara ni pamoja na ule wa Ununio kwenda Mbweni ambako ujenzi wake unaendelea kwa awamu, umaliziaji wa kipande cha barabara ya Wazo kiwandani mpaka Kisauke shule kata ya Wazo.
Wananchi wa Kilimahewa Juu katika Kata ya Wazo wilayani kinondoni, wakimshukuru Mkuu wa wilaya hiyo Daniel Chongolo  kwa kukutana nao ikiwemo sambamba na kusikiliza changamoto zinazowakabbili katika maenno yao,alkini pia kuwapa taarifa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Makongo unaotarajiwa kufanywa na Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda Ijumaa wiki hii. Picha na Michuzi JR (MMG).from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2BVQqHV
via
logoblog

Thanks for reading DC KINONDONI AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUSHUHUDIA RC MAKONDA AKIZINDUA UJENZI WA BARABARA YA MAKONGO JIJINI DAR

Previous
« Prev Post