Ticker

10/recent/ticker-posts

DC KASESELA AWATAKA WAKAZI WA WILAYA YA IRINGA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA MPIGA KURA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akinadikisha mbele ya muandikishaji wa kituo cha kinondoni 1 manispaa ya Iringa Revina Kongore
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akipata maelezo kutoka kwa muandikishaji wa kituo cha kinondoni 1 manispaa ya Iringa Revina Kongore

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa amewataka wakazi wa wilaya ya Iringa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika tarehe 24-11-2019 na kuhakikisha wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati ukifika.

Akizungumza wakati alipokuwa anajiandikisha kwenye daftari za mpiga kura katika kituo cha Kinondoni 1 manispaa ya Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa,Richard kasesela amesema kuwa kila mkazi wa wilaya ya iringa wanahaki wa kujitokeza kujiandikisha na kupata haki ya kumchagua kiongozi wanaemtaka.

“Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha unapata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kukuletea maendeleo kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha” alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwakumbusha vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha na kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi kwa kuwa nao wanahaki ya kuwa viongozi wa kuongoza mitaa ambayo wanaishi kwa maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake muandikishaji wa kituo cha kinondoni 1 manispaa ya Iringa Revina Kongore amewahimiza wakazi wa mtaa huo kuendelea kufika katika kituo na kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ili kuja kutumia haki yao ya msingi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika Tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2019 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33jU0Hh
via

Post a Comment

0 Comments