CHAMA CHA MAPINDUZI CHAELEKEZA TBA KUKAMILISHA KWA WAKATI MAJENGO YA CHUO CHA UFUNDI STADI KARAGWE

  Masama Blog      
CHAMA CHA MAPINDUZI CHAELEKEZA TBA KUKAMILISHA KWA WAKATI MAJENGO YA CHUO CHA UFUNDI STADI KARAGWE NA KUSISITIZA KWA WADHIBITI UBORA WA ELIMU NCHINI KUHUSU UMUHIMU WA HISTORIA YA NCHI KWA WATOTO WETU SHULENI

29 Oktoba 2019

Akiwa katika ziara ya ukaguzi na ufuatiliaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mwaka 2015 – 2020 Mkoani Kagera na Wilayani Karagwe Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi ameelekeza Wakala wa Nyumba wa Serikali (TBA) kukamilisha kwa wakati Majengo ya Chuo cha Ufundi Stadi Wilaya ya Karagwe ili vijana wa Kitanzania wanufaike na elimu ya Ufundi Stadi na kujiajiri. Ujenzi wa Majengo mapya tisa na ukarabati wa majengo makongwe katika chuo hicho unagharimu shilingi bilioni 4.6 ambazo zimetolewa na Serikali.

Wakati uo huo Ndugu Polepole ametembelea na kukagua jengo jipya la Ofisi ya Udhibiti Ubora wa elimu kwa Wilaya za Karagwe na Kyerwa ambalo ni sehemu ya Majengo 100 yaliyojengwa katika Wilaya mbalimbali nchini. Ujenzi wa jengo hilo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya tano inayoongoza na Rais John Pombe Joseph Magufuli katika kutoa elimu bure, kuboresha miundombinu ya kufundishia, kuweka mazingira mazuri ya kusomea, kusimamia na kuhakiki viwango vya ubora wa elimu inayotolewa katika shule zetu za msingi na Sekondari nchini sambamba na maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ndugu Polepole amehitimisha ziara yake kwa kukagua utolewaji huduma katika Kituo kipya cha Afya Kayanga na kwa kuzungumza na Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Karagwe ambako amewasisitiza kuendelea kujenga umoja, mshikamano na kutenda haki katika mchakato wa Uchaguzi wa ndani ili kujiletea ushindi mnono katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2019.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/32WyDMw
via
logoblog

Thanks for reading CHAMA CHA MAPINDUZI CHAELEKEZA TBA KUKAMILISHA KWA WAKATI MAJENGO YA CHUO CHA UFUNDI STADI KARAGWE

Previous
« Prev Post