Ticker

10/recent/ticker-posts

BALOZI KAIRUKI AYAKARIBISHA MAKAMPUNI YA SADC KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI SOKO KUBWA LA SASC NDANI YA JIMBO LA JIANGSU-CHINA

Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC kutoka Jimbo la Jiangsu umefunguliwa leo jijini Nanjing na Naibu Gavana wa Jimbo hilo Ndugu Ma Qiulin. Mkutano huo umehudhuriwa na Mabalozi 11 wa nchi za SADC na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa SADC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretariat ua SADC Bi Mapolao Mokoena.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo Balozi wa Tanzania Ndugu Mbelwa Kairuki alitoa hotuba kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wa Nchi za SADC nchini China ambapo pamoja na mambo mengine aliyakaribisha makampuni ya SADC kuchangamkia fursa za uwekezaji katika nchi za SADC kutokana  na fursa za soko kubwa la SASC lenye idadi ya watu milioni 345 na uchumi wa GDP 600 Billioni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC Bi Makolane alitoa mada kuu ambapo alielezea mazingira ya biashara na uwekezaji katika nchi za SADC. Aidha Mabalozi wa nchi za SADC walielezea fursa zilizopo katika nchi za SADC katika sekta za miundombinu, kilimo, viwanda; madini, utalii nk.  

Jiangsu ni jimbo la pili kwa ukubwa wa uchumi nchini China likiwa na GDP ya USD 1.2 Trillion na idadi ya watu milioni 80.  Jimbo hilo linaongoza nchini China katika sekta ya viwanda. Makampuni kutoka Jimbo la Jiangsu yamefanya uwekezaji nchini Tanzania katika sekta ya viwanda.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2MSwZWB
via

Post a Comment

0 Comments