ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA NDEGE LA PRECISION AAMLIWA KULIPA SH. MILIONI 12.9

  Masama Blog      
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.
ALIYEKUWA Mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Precision Air Mariethà Milinga ameamriwa kulipa fidia ya sh. Milioni 12.9 baada ya kutiwa hatiani katika shitaka lililokuwa linamkabili la kuisababishia hasara chuo kikuu huria cha Tanzania (Out).

Pia Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imemuhukumu mshatakiwa huyo kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani.

Mshtakiwa Marietha ametiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu hiyo, baada kuandika barua ya kuomba msamaha na kukiri kosa lake iliyompelekea kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

Mshtàkiwa huyo alipewa adhabu hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Agustine Rwezile.

Mshtakiwa huyo ambaye awali alikuwa akikabiliwa na mashtaka 69 yakiwemo ya utakatishaji, baada ya makubaliano hayo alisomewa shtaka moja la kuisababishia hasara mamlaka.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo mahakama iliuliza upande wa mashtaka kama wana lolote la kuongea ndipo wakili wa serikali, Jackline Nyantori aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa na kuzingatia makubaliano waliyoingia na DPP.

Katika utetezi wake, mshtakiwa Marietha ambaye alishakaa mahabusu miaka saba ameiomba mahakama isimpe adhabu kubwa kutokana na muda huo aliokaa mahabusu na pia ana mtoto mdogo ambaye ana matatizo ya Kansa.

Katika kesi hiyo, Marietha na wenzake wanadaiwa gkati ya Julai mwaka 2009 hadi Aprili 2011, waliisababishia Chuo Kikuu Huria cha Tanzanià hasara ya zaidi ya sh milioni 500.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2MXvFlr
via
logoblog

Thanks for reading ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA NDEGE LA PRECISION AAMLIWA KULIPA SH. MILIONI 12.9

Previous
« Prev Post