ALIYEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA SITA JELA, AHUHUMIWA TENA KULIPA FIDIA YA BILIONI 1.004

  Masama Blog      
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuamuru mwanasiasa  Salma Mtambo kumlipa fidia ya sh. Bilioni 1.004 Ridhuan Mringo kwa hasara aliyomsababishia kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mtambo ambaye Septemba 18, mwaka huu alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani baada ya kutiwa hatiani katika mashitaka 17 kati ya 24 yaliyokuwa yakimkabili yakiwamo ya kutakatisha fedha jumla ya Sh. 1.027,000,000, ameambiwa anapaswa kulipa fidia hiyo baada ya kumaliza kutumikia kifungo hicho.

Mshtakiwa Mtambo amesomewa adhabu hiyo ya fidia leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi Kevin Muhina ikiwa ni nyongeza ya adhabu ya kifungo ya miaka sita jela aliyopewa awali.

Kesi hiyo leo Oktoba 30, 2019 ilikuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa ombi la upande wa mashtaka lililotaka mshtakiwa alipe fidia ya kutokana na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Ridhuan Mringo.

Akisoma adhabu hiyo, Hakimu Mhina amesema fidia inakuwa ni nyongeza ya adhabu nyingine kama kifungo au mbadala wa adhabu nyingine  pale mahakama itakavyoona na kwamba  makosa yaliyomtia hatiani mshtakiwa yalimsababishia muathirika hasara ya sh bilioni 1.027.

"Kwa maoni yangu, hasara aliyoipata victim ni kubwa haiwezi kupita hivihivi hivyo mahakama kwa mamlaka yake inaona ilipwe kama nyongeza ya adhabu" amesema Hakimu

Amesema fidia hiyo ya Sh.bilioni 1.004 ilipwe mara baada ya kumaliza kifungo.Awali mshtakiwa huyo alitiwa hatiani katika mashtaka ya kuwasilisha nyaraka za uongo na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katika kosa la kugushi,  mshtakiwa Salma anadaiwa kati ya June mosi 2003 na Oktoba 31, 2011 maeneo yasiyojulikana Wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam kwa nia ya udanganyifu aligushi risiti ili kuonesha kwamba Ridhuan Mringo alinunua nyumba ya Shirika la Nyumba iliyopo Plot namba 710 mtaa wa Mfaume Upanga kwa Sh. Millioni 70 wakati akijua si kweli. 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2BXrgZv
via
logoblog

Thanks for reading ALIYEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA SITA JELA, AHUHUMIWA TENA KULIPA FIDIA YA BILIONI 1.004

Previous
« Prev Post