Waziri Jafo aipongeza Timu ya Netiboli ya Wizara hiyo, awataka kujiandaa na Muungano

  Masama Blog      
Charles James, Michuzi TV

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo ameutaka uongozi wa Timu ya Mpira wa Pete ya Wizara hiyo kuhakikisha wanafanyia kazi mapungufu yaliyopo kabla ya kwenda kushiriki mashindano ya Muungano.

Waziri Jafo amesema ni vema mapungufu yakafanyiwa kazi mapema ili wanapokwenda kwenye mashindano hayo mwezi Novemba mwaka huu wawe na timu bora itakayoweza kutwaa vikombe na zawadi mbalimbali.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wachezaji na viongozi wa Timu hiyo ambayo imekua ya nne katika mashindano yaliyomalizika Jumapili jijini Dodoma.

" Kama Waziri niwapongeze sana, mmefanya kazi kubwa na wote tumeiona. Nafasi ya nne siyo haba maana sasa tumepata nafasi ya kushiriki mashindano ya Muungano, hayo sasa naamini tunaenda kushinda vikombe na kuweka heshima.

" Lakini kama Timu tunapaswa tuanze maandalizi mapema, Novemba siyo mbali tusije tukachelewa tuangalie mapungufu yaliyoonekana kwenye mashindano haya ya Dodoma tuyafanyie kazi tuende Zanzibar tukiwa kamili.

" Najua mnaweza kuona haja ya kuongeza nguvu kwa kufanya usajili, niwasihi msisite kufanya hivyo, maana malengo yetu ni kwenda kufanya vizuri na kuwaonesha kuwa TAMISEMI na sisi tupo vizuri, " amesema Mhe Jafo.

Waziri Jafo pia ameagiza kupatiwa kiasi cha Sh Laki Tano hadi Milioni Moja kwa kila mchezaji lengo likiwa kuongeza motisha na hamasa kwa namna walivyopambana kwenye mashindano yaliyoisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wachezaji wa Timu ya Netiboli ya Wizara hiyo baada ya kumaliza mazungumzo ya pamoja  ofisi kwake jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh Selemani Jafo akizungumza na wachezaji na viongozi wa Timu ya Netiboli ya Wizara hiyo ofisini kwake jijini Dodoma


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2LBiKDZ
via
logoblog

Thanks for reading Waziri Jafo aipongeza Timu ya Netiboli ya Wizara hiyo, awataka kujiandaa na Muungano

Previous
« Prev Post