Wakala wa Tigo Pesa Tanzania wazidi kupata mafanikio

  Masama Blog      


Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni mbili, Mshindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’, Said Khatibu kutoka Zanzibar. Promosheni hii ilifanyika mwezi wa nne, mwaka huu.

Bwana Said Issa Khatib,alianza safari yake ya kuelekea kwenye mafanikio kwa kutumia kadi ya simu ya kuazima kutoka kwa jirani yake mwaka 2014, kwa sasa ni moja kati ya mawakala wakubwa zaidi wa Tigo Pesa, mjini Zanzibar. Biashara imekua kutoka ilivyokuwa mwanzoni na kufikia kufanikiwa kukuza biashara yake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kufikia kuwa biashara ya mamilioni, jambo ambalo liliwezeshwa na idadi ya wateja inayoongezeka kila siku ya wateja wa Tigo Pesa.

Bwana Khatib ambaye pia ni mshindi wa tuzo nyingi za Tigo Pesa zenye jumla ya milioni 15/- katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, alisema kwamba alianza biashara yake kwa kutumia line ya simu aliyoazima kutoka kwa jirani yake. Kama ilivyo kwa maelfu ya mawakala wengine waliosambaa nchi nzima, Khatib aliona fursa kubwa katika biashara ya kampuni ya simu ya Tigo ya kuhamisha pesa baada ya kujipatia line yake mwenyewe ya Till ya Tigo Pesa miaka mitano iliyopita.

"Nilitumia line ya jirani yangu kwa muda wakati huo nikiwa natunza pesa kwa ajili ya kuweza kupata line yangu mwenyewe. Nilikuwa nampa jirani yangu asilimia 70 ya mapato ya siku wakati mimi nakibakiwa na asilimia 30", bwana Khatib ambaye ni baba wa watoto watatu alisema wakati akibainisha kwamba mpango wake ulikuwa ni kuwa super dealer wa kampuni ya Tigo mjini Zanzibar, kampuni ya huduma za simu za mkononi inayokua kwa kasi zaidi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ZVypTy
via
logoblog

Thanks for reading Wakala wa Tigo Pesa Tanzania wazidi kupata mafanikio

Previous
« Prev Post