WAHITIMU SHAHADA ST. JOSEPH, TANZANIA WASAFIRISHWA ITALIA KWA MASOMO YA URUSHAJI SATELLITE YA KWANZA NCHINI

  Masama Blog      

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Wahitimu wawili wa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Tanzania (Bachelor in Electronics and Communications Engeneering) wamesafiri kuelekea nchini Italia katika Chuo Kikuu cha Parma kuendelea na masomo yao ya Shahada ya Uzamili.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3), Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Innocent Ngalinda amesema Wanafunzi hao wanaenda Italia kujifunza namna yakurusha Satellite wakati Tanzania ikijiandaa kufanya hivyo, amesema hivi karibuni Wanafunzi wengine Kumi wataelekea India kujifunza masuala hayo.

Prof. Ngalinda amesema Wahitimu wengine wataenda nchini India kujifunza masomo hayo yaurushaji wa Satellite angani, kutokana na India kuongoza katika kurusha Satellite nyingi duniani.

Pia amesema Wahitimu hao wanaenda masomoni Italia ikiwa ni mpango wa ushirikiano wao na Vyuo vya nje ya nchi katika kuwapeleka Wanafunzi kusoma masuala mbalimbali bila gharama yoyote kuhakikisha Tanzania inafika katika Uchumi wa Viwanda kwa vitendo.

Prof. Ngalinda amewataka Wanafunzi wengine chuoni hapo kusoma kwa bidi ili kufika malengo yao kwa wakati sahihi kama walivyofanya wenzao wanaoelekea Italia na India.

Kwa upande wa Penina Mbwilo ambaye ni mmoja wa Wahitimu wa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Tanzania amesema ilikuwa ndoto kwake kumaliza masomo ya Shahada nakuendelea na masomo ya juu zaidi.

Penina amewaasa Wanafunzi wenzake kusoma kwa bidii sambamba nakufaulu vizuri darasani ili kufikia malengo yao kama yeye alivyofikia, amesema pia ili kufika malengo hayo Mwanafunzi anapaswa kujiongeza katika masomo yake, nidhamu na utii.Amesema malengo yake kupata ujuzi zaidi na kuwasaidia wengine katika ujuzi huo kwa kuwafundisha ili na wao kupata nafasi kama aliyopata yeye.

Naye Frank Charles aliyehitimu Shadaha hiyo ameshukuru kupata nafasi hiyo kuelekea kusoma nje ya nchi sambamba na kuongeza ujuzi katika msomo hayo ambayo yatasaidia Taifa, pia amesema anaenda kujifunza kwa Mataifa mengine masuala ya mawasiliano namna ambavyo mataifa hayo yameendelea katika Sekta hiyo.

Wahitimu hao wanaelekea nchini Italia katika Chuo Kikuu cha Parma kutokana na kusoma, ufaulu mzuri katika masomo yao hivyo kuchaguliwa kuwakilisha wengine nchini humo. Wahitimu wengine wanaelekea nchini India kwa masomo hayo na kurusha Satellite ya kwanza nchini Tanzania.
Penina Mbwilo ambaye ni mmoja wa Wahitimu wa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya safari yao
Frank Charles aliyehitimu Shadaha hiyo akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya safari yao ya nchini Italia katika Chuo Kikuu cha Parma kwa ajili ya masomo.
Wahitimu wawili wa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Tanzania (Bachelor in Electronics and Communications Engeneering) wakiwa katika picha ya pamoja na Ndugu, Jamaa na marafiki kabla ya safari.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2LENVy1
via
logoblog

Thanks for reading WAHITIMU SHAHADA ST. JOSEPH, TANZANIA WASAFIRISHWA ITALIA KWA MASOMO YA URUSHAJI SATELLITE YA KWANZA NCHINI

Previous
« Prev Post