RAIS WA NIGERIA KUTEMBELEA AFRIKA KUSINI BAADA YA KUVURUGIKA UHUSIANO KUTOKANA NA VURUGU

  Masama Blog      
Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria atatembelea Afrika Kusini kwa ziara ya kikazi  kujaribu kuboresha uhusiano uliovurugika wa nchi mbili kufuatia wimbi la ghasia na mashambulizi yaliowalenga wageni katika nchi hizo mbili.

Mgogoro wa kidiplomasia umezuka baina ya Afrika Kusini na Nigeria baada ya magenge ya watu kushambulia wageni huko Afrika Kusini, na matokeo yake wananchi wa Nigeria nao kushambulia vituo vya biashara vinavyomilikiwa na raia wa Afrika Kusini nchini mwao. 

Afrika Kusini imefunga ubalozi wake nchini Nigeria baada ya Nigeria nayo kumuita nyumbani balozi wake nchini Afrika Kusini.

Mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni huko Afrika Kusini yameibua hasira kote barani Afrika ambapo maduka yanayomilikiwa na mashirika ya Afrika Kusini yameporwa nchini Nigeria.
 
Mashirika makubwa ya Afrika Kusini ya Shoprite na MTN yamelazimika kufunga maduka yao kote Nigeria kufuatia mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Siku ya Alhamisi Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini alisema watu wasipungua 10 wameuawa katika ghasia za hujuma dhidi ya raia wa kigeni nchini humo.


from CCM Blog https://ift.tt/2N3S6Xe
via
logoblog

Thanks for reading RAIS WA NIGERIA KUTEMBELEA AFRIKA KUSINI BAADA YA KUVURUGIKA UHUSIANO KUTOKANA NA VURUGU

Previous
« Prev Post