Ticker

10/recent/ticker-posts

Programu ya Vodacom Digital Accelerator yazinduliwa jijini Dar




Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia Vodacom imeshirikiana na kampuni ya Smart Codes. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Smart Codes, Edwin Bruno

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Smart Codes, Edwin Bruno (Kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Rosalynn Mworia, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia ( Smart lab) Vodacom imeshirikiana na kampuni ya Smart Codes.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi (katikati) na Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia (Kushoto), wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Smart Codes, Edwin Bruno wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia. Codes.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia ( Smart lab) hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc imeshirikiana na kampuni ya Smart Codes.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi akipiga picha "selfie" na wadau pamoja na wageni waalikwa kwenye tafrija mchapalo ya uzinduzi wa programu ya Vodacom Digital Accelerator
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi akizungumza kwenye hadhara ya tafrija mchapalo ya uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia, Vodacom imeshirikiana na kampuni ya Smart Codes.

Wafanyakazi wa Vodacom wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa programu ya Vodacom Digital Accelerator jijini Dar Es Salaam jana.



Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi inayoongoza Vodacom Tanzania Plc na Smart Lab leo wamezindua kampeni ya “Vodacom Digital Accelerator,” programu yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato.


Programu hii ambayo itakuwa inafanyika kila mwaka ina lengo la kubainisha na kusaidia wajasiriamali wanaochipukia katika sekta ya simu, mawasiliano, teknolojia katika taasisi za kifedha, habari, afya, elimu na biashara ya mtandao (E-commerce) watakuwa na hatua tatu ambazo zinajumuisha kutuma maombi, kuchaguliwa na hatua ya kuongeza kasi ya biashara (Mchapuo).

Akiongea katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Bwana Hisham Hendi amesema kwamba ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania na SmartCodes ni hatua muhimu kuelekea katika kutoa fursa kwa wajasiriamali wanaoanza kwa kupitia sekta ya teknolojia ambayo itapelekea kuwepo kwa mifumo inayofanya kazi ambayo itanufaisha jamii, hususani kwa vijana nchini. Amewahamasisha vijana wengi zaidi kuwa wabunifu na kutumia fursa hii kama njia ya kujiwezesha kiuchumi kupitia katika kutatua matatizo ya maendeleo ya jamii katika jamii zao.

“Kampuni ya Vodacom mara zote inakusudia kuleta mabadiliko endelevu yenye manufaa kwa jamii ambako tunaendesha shughuli zetu sambamba na mtazamo wa mkakati wetu wa kibiashara na programu ya Vodacom Accelerator inakusudia kuthibitisha suala hilo.” Aliongeza bwana Hisham.

Alifafanua zaidi kwamba kama kampuni ambayo inakusudia kufikisha Tanzania katika ulimwengu wa kidigitali, kampuni ya Vodacom Tanzania inahamasisha fikra za biashara katika sekta ya teknolojia ambazo zitaleta mabadiliko endelevu.

“Teknolojia ya Digitali haibadilishi namna tunavyofanya biashara Afrika tu bali pia inabadilisha tunavyotazama na kutatua masuala yanayohusu maendeleo. Kwa hiyo ni kwa heshima kubwa kwamba tutatengeneza fursa ya kutambua fikra kama hizo, kuziunga mkono na kuziboresha kwa lengo la kukuza manufaa yake katika jamii, Alisema.

Aliongeza pia, Vodacom imeshirikiana na Smart Lab, kituo maarufu cha ubunifu ambacho kinakusudia kuleta matokeo halisi ambayo yatabadilisha mwelekeo wa ubunifu wa mifumo ya kiuchumi. Kwa hiyo, hii itakuwa ni fursa kwa wafanyabiashara wanaoanza na wavumbuzi katika vigezo vya kiteknolojia vilivyochaguliwa kuonyesha bidhaa zao na kunufaika kutokana na programu hii ikiwemo kupata mpango wa ushirikiano na kampuni ya Vodacom, ushauri, msaada wa kitaalamu, masoko na fursa ya kupata nafasi ya kuwa karibu na mtandao mkubwa wa washirika wa kampuni za Vodacom na Smart Lab na hatimaye wateja kuweza kufanya majaribio na kupata uzoefu wa masuluhisho yao.



Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Smart Codes bwana Edwin Bruno ameonyesha furaha yake kuhusu programu hii mpya kwa kusema kwamba, “Tunafuraha kuwa sehemu ya programu ya “Vodacom Accelerator” na kwa kushirikiana na Vodacom, kwa pamoja tunatumaini kutengeneza jukwaa la chapa ya kipekee kwaajili ya vijana wenye ari katika teknolojia. Progamu hii inaenda sambamba na mkakati wetu wa shirika wa kupeleka ujumbe kuhusu kusaidia vijana walioko katika zama za digitali na tunashukuru kwa Vodacom Tanzania ambao wameona haja ya kutengeneza mzunguko mpya wa hadithi za mafanikio ya wajasiriwamali wa kiafrika wanaojenga kampuni za teknolojia zinazokuwa kwa kasi ambao wanatoka ndani ya nchi.”

Alieleza kwa kina kwamba “jamii ya wavumbuzi na wabunifu imeibuka nchini Tanzania kutoka katika vituo vichache mwaka 2011 mpaka kufikia zaidi ya 45 mwaka 2019. Lakini kumekuwa na ushirikishwaji mdogo kutoka katika upande wa mashirika ambapo kampuni ya Vodacom katika ushirikiano huu na kampuni ya Smart Lap itaongoza katika kuziba pengo hilo. Tunatazamia katika zama zijazo za ushirikishwaji wa teknolojia kwa Tanzania ambayo ina mifumo yenye kuleta mabadiliko ambayo italeta manufaa kwa kizazi kijacho.”

Katika kipindi cha programu ambapo pia kina lengo la kuongeza rasilimali za shirika, mtandao, washauri, na washirika, washiriki watawasilisha maendeleo ya mifumo yao kwa jopo la wawekezaji na washiriki wengine katika mwisho wa kipindi cha miezi mitatau ya kuongeza kasi, ambapo mshindi atapata msaada zaidi kutoka Vodacom Tanzania Plc, Smart Lab na washirika wake kwa muda wa nyongeza wa miezi 6.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Rosalynn Mworia alisema kwamba kampuni ya Vodacom imewekeza zaidi ya dola za kimarekani 150,000 katika mpango huu ili kusaidia vijana kielimu na utaalamu kusudi waweze kufikia malengo yao ya kibiashara.

Kampuni ya Vodacom Tanzania inaongoza katika mageuzi ya sekta ya teknolojia Tanzania (fintech) ambayo ni moja ya sekta zinazokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika. Na wakati huo huo teknolojia ikiwa inaendelea kusaidia uendeshaji wa kila siku wa biashara na huduma.

Uzinduzi pia ulihudhuriwa na wadau wengine kutoka serikalini, jamii ya wawekezaji, vituo vya uvumbuzi, taasisi za kifedha, mashirika, wafanyabiashara chipukizi, maprofesa wa vyuo vikuu, washirika wa maendeleo, Mabalozi na watendaji wengine katika teknolojia na jamii ya wavumbuzi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Q2CMNb
via

Post a Comment

0 Comments