MTANDAO WA YOUTUBE WAFUTA MAONI MILIONI MIA TANO

  Masama Blog      
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MTANDAO wa Youtube umeendelea na jitihada zake na kulingana na matamshi yenye chuki ambapo mapema katika awamu ya pili ya utakatishaji wa maudhui, mtandao huo umeondoa maoni milioni 500 ikiwa ni kutekeleza sheria hasa katika kupambana na matamshi ya chuki katika mtandao.

Kupitia blog ya mtandao huo imeelezwa kuwa maoni yenye chuki yameongezeka mara mbili ya maoni yaliyoondolewa awamu ya kwanza, pia picha mjongeo (video) laki moja zenye matamshi yenye chuki zimefutwa huku chaneli elfu kumi na saba zikibainika kuvunja sheria kwa kuweka matamshi yenye chuki katika chaneli zao.

Mkurugenzi wa mtandao huo Susan Wojcicki  ameeleza kuwa uwazi wa kutoa maoni katika mtandao wa Youtube utaendelea ila wataendelea kupiga vita maudhui yanayovunja sheria.

Kutokana na kuendelea kuchapishwa kwa maandiko na picha zenye chuki katika mtandao wa Youtube mwezi Juni mwaka huu walizifungia video ambazo zilikiuka sheria na kuwa na maudhui yenye chuki, udini, ubaguzi wa kijinsia na ukabila.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Q1konH
via
logoblog

Thanks for reading MTANDAO WA YOUTUBE WAFUTA MAONI MILIONI MIA TANO

Previous
« Prev Post