Ticker

10/recent/ticker-posts

KUUNDWA KWA JUKWAA LA WADAU SEKTA YA SHERIA KUTALETA MAENDELEO KATIKA TAIFA-KATIBU MKUU.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg George J. Kazi akitowa maelezo kuh kuanzishwa kwa Jukwaa la Sheria Zanzibar 
Muwezeshaji kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar Ndg Mohammed Khamis akitoa mada kuhusu taarifa ya utafiti juu ya uwezekano wa kuanzisha jukwaa la pamoja kwa wahusika sekta ya sheria Zanzibar 

Na Raya Hamad - WKS 

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg George Joseph Kazi amesema kuundwa kwa jukwaa la wadau wa sekta ya sheria kutasaidia kuwaunganisha wadau wa sekta hio na kuleta maendeleo endelevu katika kada hio muhimu kwa maslahi yaTaifa 

Ameyasema hayo kwenye mkutano uliowakutanisha viongozi na watendaji kutoka sekta ya sheria uliojadili taarifa ya utafiti juu ya uwezekano wa kuanzisha jukwaa la pamoja kwa wahusika washeria Zanzibar 

George Kazi amewataka wajumbe hao kutoa michango na mawazo yao na kufanya upembuzi ili kuona mahitaji muhimu yatakayosaidia kufahamu sekta ya sheria, kwa kutambuwa kuwa sekta ya sheria ndio kiini katika masuala yote ya maendeleo ya nchi . 

Mbali ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu , Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Tume ya kurekebisha Sheria na Mahakama lakini kumekuwa na ongezeko kubwa la wanasheria hata hivyo kinachokosekana ni kutokuwa na jukwaa la pamoja linalowaunganisha wanasheria hao 

Jukwaa ambalo litasimamia na kuangalia maendeleo ya sekta ya sheria hali ilivyo na jinsi gani itakuwa na uratibu ambao utasaidia kujuwa mambo mengi ya kuangalia wapi tulipotoka ,tulipo na tunakoelekea, matatizo gani yanayoikumba sekta sheria iwe ya Jinai na Madai kwa ajili ya maendeleo chanya ya sekta ya hio 

Katibu George amesema sekta ya sheria inaendelea kukuwa kwa kasi hivyo wizara imeona ipo haja ya kuwa na chombo ambacho kitasaidia kuzidisha kasi ya uwajibikaji ili kila mmoja atimize wajibu wake “muhimu kujielewa kama wanasheria kufahamu jukumu walilonalo na kazi wanazozifanya ikiwemo kufanya tathmini ya kile wanachokifanya badala ya kufanya kazi kwa mazoea, hii itasaidia kuleta chachu katika sekta ya sheria kujenga utamaduni wa kujisomea na kufahamu mambo mapya yanayotokea hivyo jukwaa hili litatusaidia tuweze kujitambua”alisema George 

Ameendelea kusema kuwa kupitia Jukwaa upo uwezekano wa kufanya utafiti na kufahamu kiwango cha ongezeko la wanasheria, kuwafahamu mawakili na mahakimu na kuona sekta ya sheria imekuwa kwa kiwango gani na je ni kweli wamebobea kuwa wataalamu wanaofikia kiwango na vigezo vinavyohitajika katika kada ya sheria 

Kuwepo kwa Jukwaa moja litawezesha pia kutoa mapendekezo na kuwasilisha taarifa zao ambazo zitapelekea Wizara kuweza kuzifanyia kazi kwa pamoja . 

Nao wawasilishaji kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ndg Mohammed Khamis na ndugu Mussa Kombo wamesema lengo la kuwa na chombo hiki nikusaidiana mawazo na ushauri ilikuona uwajibikaji unaimarika na sio kuingilia majukumu yaVyombo vya kisheria pia kuondosha migongano ya kisheria baina ya taasisi na kutekelezwa kwa vitendo mawazo na ushauri utakaotolewa . 

Nae Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar ndugu Ibrahim Mzee Ibrahim ameanisha mambo manne ambayo yakitekelezwa ipasavyo yatakuwa nichachu yamaendeleo ikiwemo vyombo vya mashtaka kufahamu majukumu yao yakiutendaji, pia kufuatwa kwa Maadili na taratibu zake, usimamizi pamoja na suala la uwajibikaji na ushirikiano baina ya vyombo vya Sheria vilivyopo nchini. 

Aidha amesema kinachounganisha taasisi hizi zote za sheria ni muongozo wa taasisi na kila chombo kinamamlaka yake na imewekewa sheria hivyo kuwepo kwa jukwaa hili kutasaidia kuondosha baadhi misuguano na kuwa na sauti ya pamoja katika utekelezaji wa masuala ya utowaji haki na sheria na mwisho wa yote ni taasisi yenyewe iliyopewa mamlaka kuona vipi inabadilika kwa kufuata taratibu 

Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Bi Daima Mohamed Mkalimoto amewataka wawasilishaji ya mada kuyapitia majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na bajeti ya Wizara ili kujenga hoja kwa msingi imara itayosaidia kuundwa kwa kwa jukwaa la pamoja . 

Bi Daima ametoa mapendekezo kwa kuona tunaanajifunza pia mazuri yanayotekelezeka kutoka kwa wengine na kusema kuwa uhai wa sekta ya sheria utaonekana kwa kuangalia zaidi na kuona umuhimu wa kuweka jukumu la kulinda rasilimali za nchi kuangalia mikataba kiundani kutoa mapendekezo pia kuweka uwiyano katika jamii hata katika ngazi za Mikoa na Wilaya ili na wao waweze kuangalia masuala ya kisheria katika maeneo yao 

Kamishna wa Kazi Bi Fatma Iddi Ali amesema kuundwa kwa Jukwaa la pamoja kwa sekta ya sheria hakutakuwa na muingiliano bali ni kuondoa ukakasi lakini utazingatia umuhimu wa taasisi zinazoguswa kwani kila taasisi inayosimamia sheria ina taratibu zake namiongozo yake ya kiutendaji 

Aidha amesisitiza juu ya namna yakumuandaa na kumuuangalia mwanasheria na kazi anazozifanya ili aweze kuwa na maadili mazuri anakoelekea kwa vile mwanasheria ndie anaetegemewa kuwa Jaji, Mrajisi wa mahakama , Hakimu, Wakili ama kwa namna yeyote kuwa msimamizi katika masuala ya sheria na utowaji wa haki 

Bi Hamisa Mmanga Makame Mkurugenzi mipango uendeshaji na rasilimaliwatu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ameipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kutokana na jitihada zilizopo ukilinganisha na miaka yanyuma hivi sasa kila siku kunapiga hatua na maendeleo yanaonekana kupitia sekta ya sheria 

Wakili wa Mahakama kuu Zanzibar Bw Zaharani Mohamed Yussuf ametoa msisitizo kushirikishwa kikamilifu kwa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana ambao nao wanasimamia utatuzi wa migogoro, mali hivyo kuwepo kwachombo hiki kutarahisisha utowaji wa haki kwaupande wao na kwa wanajamii . 

Mkutano huo uliowakutanisha viongozi na watendaji kutoka sekta ya sheria uliojadili taarifa ya utafiti juu ya uwezekano wa kuanzisha jukwaa la pamoja kwa wahusika wa sekta ya sheria Zanzibar umeandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Shirika la Mendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP umefanyika kwenye ukumbi wa mkutano uliopo Zanzibar Beach Resort Mazizini. 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2PXyTc9
via

Post a Comment

0 Comments