HISTORIA YA CCM KWA UFUPI

  Masama Blog      
Historia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilianza rasmi Februari 5, 1977 kutokana na kuunganishwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa chama tawala Tanzania Bara, kikiongozwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala Zanzibar kikiongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh  Amaan Abeid Karume.

Itikadi
Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha.

Kutokana na Azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hiyo pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.

Uchaguzi
CCM imekuwa ikishinda chaguzi za Urais toka mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa nchini Tanzania huku pia kikipata idadi kubwa ya wabunge wa Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi.

Baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi CCM imeendelea kuiongoza Tanzania kutokana na kushinda chaguzi zilizofanyika tangu1995. Viongozi walioweza kushinda kwa tiketi ya CCM kwenye chaguzi hizo ni Benjamin Mkapa,Jakaya Mrisho Kikwete na Dk. John Joseph Pombe Magufuli.

Viongozi walioshika Uenyekiti wa CCM miaka waliyoongoza ikiwa kwenye mabano, ni;
1. Julius Nyerere (1977 - 1990)
2. Ali Hassan Mwinyi (1990 - 1996)
3. Benjamin Mkapa (1996 - 2006)
4. Jakaya Kikwete (2006 - 2016)
5. John Pombe Magufuli (2016 hadi sasa)

Jumuiya
CCM inazo Jumuiya tatu ambazo zinafanyakazi kwa kuyaunganisha makundi ya Vijana (Umoja wa Vijana wa CCM), Wanawake (Umoja wa Wanawake Tanzania- UWT) na Jumuiya ya Wazazi Tanzania. Jumuiya hizi kila moja ina viongozi ambao moangilio wake unafanana na ule wa CCM yenyewe kuanzia ngazi ya Mwenyekiti Taifa hadi ngazi za matawi.

from CCM Blog https://ift.tt/2A0fIna
via
logoblog

Thanks for reading HISTORIA YA CCM KWA UFUPI

Previous
« Prev Post