ZARIF: MELI YA MAFUTA YA IRAN ILIKUWA IMEZUIWA KINYUME CHA SHERIA

  Masama Blog      
Katika ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa Twitter Alhamisi usiku, Zarif ameambatanisha nakala mbili za barua ambazo ubalozi wa Iran mjini London umeiandikia Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza na kusema: "Ubalozi wa Iran mjini London umelalamika kuhusu kushikiliwa kinyme cha sheria Meli ya mafuta ya Grace 1 na umeifahamisha Wizara ya Nje ya Uingereza kuwa, vikwazo vya Umoja  wa Ulaya havihusu Iran na huu ni msimamo wa aghalabu ya nchi za Ulaya."
Baada ya Jeshi la Majini la Uingereza kutekeleza uharamia na kuiteka meli ya mafuta ya Iran inayojulikana kama Grace 1 katika eneo la Jabal al Tariq (Gibraltar) mnamo Julai 4, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilikuwa imedai kuwa hatua hiyo ililenga kutekeleza vikwazo vya Umoja wa Ulaya. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa hatua hiyo ya Uingereza ilikuwa kinyume cha sheria


from CCM Blog https://ift.tt/2H8j2kj
via
logoblog

Thanks for reading ZARIF: MELI YA MAFUTA YA IRAN ILIKUWA IMEZUIWA KINYUME CHA SHERIA

Previous
« Prev Post