Ticker

10/recent/ticker-posts

YANGA KUCHEZA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI KABLA YA KUWAVAA WABOTSWANA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kikosi cha Yanga kimesafiri asubuhi ya kuelekea Nyanda za juu kaskazini Kilimanjaro kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers utakaopigwa nchini Botswana.

Akizungumza na waandishi wa habari  Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Mwakalebela amesema Kikosi chao kimeamua kuweka kambi mkoani Kilimanjaro ili kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa August 23.

Amesema mazingira ya nchini Botswana yanalingana na hali ya hewa ya Kilimanjaro kwahiyo wameonelea timu ikakae huko kwa muda pamoja na kucheza mechi mbili za kirafiki.

Mwakalebela amesema, watacheza mchezo wa kwanza na Polisi Tanzania iliyopanda ligi kuu msimu huu na pia watacheza mechi ya pili na AFC Leopard ya nchini Kenya ambayo ina historia kubwa na klabu yao katika miaka ya 1970 mechi iliyofanikisha kujenga jengo la Mtaa wa Mafia.

“kuelekea kwenye mchezo wa marudiano ya timu ya Township Rollers, kikosi kitaendelea na mazoezi na pia tutacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania (August 16) na AFC Leopards (August 18),”amesema Mwakalebela.

Amesema Kocha Mkuu Mwinyi Zahera ameuhakikishia uongozi kuwa wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Rollers na watahakikisha wanapata matokeo ugenini na kufuzu raundi ya kwanza.

Katika hatua nyingine Mwakalebela amesema wamefanya mawasiliano na CAF  ili waweze kupata  leseni za wachezaji wao watatu kabla ya kwenda kwenye mchezo wa marudiano nchini Botswana

Amesema lengo la Yanga ni kuhakikisha wanakwenda Botswana wakiwa na kikosi chao kamili.

Wachezaji  waliukosa mchezo wa kwanza ni mlinda mlango Farouk Shikalo, Moustafa Suleiman na David Molinga.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2N4z4zv
via

Post a Comment

0 Comments