Waziri Simbachawene apiga stop vifungashio vya Plastiki

  Masama Blog      
*Ataka wafanyabiashara wafuate sheria

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.

Serikali imesema kuwa sheria ya zuio ya mifuko ya Plastiki itekelezwe kwa wafanyabiashara kwa kuacha kuuza vifungashio ambavyo ni vibebeo vya bidhaa mbalimbali.

Hayo aliyasema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene wakati alipotembelea soko la Kariakoo kwa wafanyabiashara wa mifuko waliomuomba kupata ufafanuzi wa mifuko na vifungashio katika Soko hilo jijini Dar es Salaam.

Waziri Simbachawene amesema kuwa wafanyabiashara kuacha kununua vifungashio kwa wazalishaji kutokana vifungashio hivyo havina utofauti na mifuko ya Plastiki.

Amesema sheria hata yeye inamfunga akikutwa na vifungashio hivyo ambavyo bado ni mifuko ya plastiki iliyowekewa marufuku tangu Juni Mosi mwaka huu.

Amesema vifungashio ambayo vinahitajika ni vile yenye lakiri alama na mfanyabiashara aonyeshe namna ya kufanya vifungashio hivyo kuweza kurudi mara baada ya kutumia ili kusiwepo na uharibifu wa Mazingira.

Nae Mwanasheria wa NEMC Heche Suguta amesema kuwa sheria imeshaeleza na hakuna kurudi nyuma kinachotakiwa ni utekelezaji wa sheria hiyo kwa wadau wote.

Amesema kuwa faini na vifungo vilishaelezwa hivyo mifuko ya plastiki ambayo inadaiwa vifungashio viondolewe katika mzunguko.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene akionesha mifuko inayodaiwa vifungashio wakati bado inajulikana no mifuko ya Plastiki iliyopigwa marufuku kuanzia Juni Mosi Mwaka huu katika mkutano na wafanyabiashara hao jijini Dar es Salaam.Kulia ni kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Baraza laTaifa la  Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Heche Suguta.
 Mwanasheria wa NEMC Heche Suguta akizungumza namna sheria inavyotekelezeka katika marufuku ya mifuko ya Plastiki wakati walipokutana na wafanyabiashara wa mifuko katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene akitoa ufafanuzi wa sheria ya mifuko ya Plastiki alipokutana na wafanyabiashara ya mifuko katika Soko dogo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene akiangalia vifungashio vidavyodaiwa ni Plastiki kutokana na sheria ya marufuku ya mifuko ya Plastiki.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene akioneshwa mfuko ya kubebea taka na mfanyabiashara katika Soko dogo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2YTU5Ur
via
logoblog

Thanks for reading Waziri Simbachawene apiga stop vifungashio vya Plastiki

Previous
« Prev Post