Waziri Jafo kufungua mkutano mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri

  Masama Blog      

Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh Suleiman Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri utakaofanyika jijini Dodoma kuanzia Agosti 20 hadi 24 Mwaka huu.

Akizungumzia mkutano huo Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe wa TAMISEMI, Dk Ntuli Kapologwe amesema kauli mbiu ya mkutano huo itakua ni uajibikaji ni nguzo muhimu katika utoaji huduma bora za afya kuelekea uchumi wa kati.

Amesema mkutano wa mwaka huu utakua ni tofauti na mikutano mingine kutokana na kuanzisha ushirikiano wa karibu baina yao na Wizara ya Afya huku pia wakiwakaribisha Wakurugenzi wa Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali Maalum ya Jakaya Mrisho Kikwete, Wakurugenzi wa Hospitali za Kanda na wadau wengine.

" Ukiachia hao pia tutakua na Makatibu wa Afya wa Mikoa na moja ya vitu tutakavyofanya katika mkutano huu ni kufanya tathimini ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita kuhusiana na utekelezaji wa afua mbalimbali za sekta ya Afya lakini ukiachia hivyo tutafanya pia tathimini ya kuangalia maazimio tuliyoingia mwaka jana kuangalia jinsi gani tulivyoyatekeleza," amesema Dk Kapologwe.

Amesema sambamba na hayo wataeka mikakati kwa ajili ya mwaka mwingine ujao ambao pia wataufanyia tathimini Agosti 2020.

Dk Kapologwe amesema mkutano huu pia utakua tofauti kwa sababu watapokea zaidi mawasilisho yatakayotoka katika ngazi za Mikoa na Halmashauri.

" Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri wana changamoto mbalimbali na wana mambo waliyofanya vizuri. Wao ndio watakua watoaji mada na sisi tutakua wachangiaji lakini ukiachilia hilo Wizara ya Afya kama watengenezaji Sera watakua na jukumu la kuwasilisha mada mbalimbali za kisera ambapo Waganga wakuu na Wakurugenzi wa Hospitali watahakikisha wanazipeleka katika maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji," amesema Dk Kapologwe.

Aidha amesema watatumia njia mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za kina juu ya kile kinachojiri kwenye mkutano huo ambapo watatumia tovuti ya TAMISEMI, Mitandao ya kijamii sambamba na vyombo vya habari lengo ni kuwafanya pia wananchi washiriki katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe TAMISEMI, DK Ntuli Kapologwe akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na mkutano mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri utakaofanyika Jijini Dodoma


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2TIMYbS
via
logoblog

Thanks for reading Waziri Jafo kufungua mkutano mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri

Previous
« Prev Post