WALIOFARIKI AJALI YA MOTO MOROGORO WAFIKIA 75

  Masama Blog      
Majeruhi wanne kati ya 43 wa ajali ya Lori lililolipuka Morogoro waliohamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamefariki  na kufanya idadi ya waliofariki kufika 75 huku 39 waliobaki wakiendelea kupatiwa matibabu.

Taarifa hii imetolewa na mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha.
 
Kuhusu hali za majeruhi mkuu huyo wa kitengo cha mawasiliano amesema wanaendelea vizuri na wapo wanaoonyesha matumaini.

“Tumepoteza wenzetu wengine wanne na miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hivyo kama kuna ndugu wa karibu waje kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao,” amesema Aligaesha.


from CCM Blog https://ift.tt/2YLur4n
via
logoblog

Thanks for reading WALIOFARIKI AJALI YA MOTO MOROGORO WAFIKIA 75

Previous
« Prev Post