Vodacom ilivyoshiriki maonesho ya Nane nane mkoani simiyu na jijini Arusha

  Masama Blog      


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akimkabidhi tuzo Mkuu wa mauzo wa kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa kampuni bora upande wa mawasiliano kanda ya kaskazini katika maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika jijini Arusha, hivi karibuni, kushoto kwa Ulega ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (mwenye kofia). Kampuni ya Vodacom Tanzania inaendelea kuboresha huduma zake kuwa za kidijitali ili kuwawezesha Watanzania kwenda sambamba na maendeleo ya ulimwengu.
Mtaalamu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Mandela Seth, akiwapa maelezo ya kutumia kifaa cha intaneti (modem) wateja waliotembelea banda la Vodacom katika viwanja vya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu hapo jana. katika maonyesho ya nane nane mwaka huu kampuni ya Vodacom imewandalia wateja wao huduma za kidigatili ikiwemo vifaa mbali mbali vya intaneti na simu.
Wakazi wa Bariadi mkoani Simiyu wakipatiwa huduma mbalimbali kwenye banda la Vodacom katika viwanja vya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu hapo jana. katika maonyesho ya nane nane mwaka huu kampuni ya Vodacom imewandalia wateja wao huduma za kidigatili ikiwemo vifaa mbali mbali vya intaneti na simu.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/31HfAVE
via
logoblog

Thanks for reading Vodacom ilivyoshiriki maonesho ya Nane nane mkoani simiyu na jijini Arusha

Previous
« Prev Post