Ticker

10/recent/ticker-posts

TAKUKURU MKOA WA DODOMA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 135


Na EZEKIEL MTONYOLE, DODOMA.

Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU] Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amesema kwa kipindi cha miezi sita wamefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi, Milioni 135, zilizokuwa zipotee kwa katika miradi mbalimbali.

Akizungumza na Fullshangwe Blog, mapema leo Agosti 13,2019 Ofisini kwake jijini Dodoma, amesema Fedha hizo zimeokolewa kwa kipindi cha Miezi 6 kuanzia Mwezi Januari,hadi Juni ,2019.

“Kwa kipindi hicho pia tumefanikiwa kudhibiti zaidi ya sh.Milioni 322, na kunzia Januari hadi Juni ,2019 tumepokea jumla ya Malalamiko 231 ya vitendo vya rushwa” amesema.

Bw.Kibwengo amesema asilimia 28% ya Malalamiko hayo yanatoka Serikali za mitaa[TAMISEMI],Ardhi kwa asilimia 26.5%,Polisi 7% na mahakama malalamiko kwa asilimia 6% na asilimia zilizobaki ni kwa sekta nyingine, huku akiitaja wilaya ya Dodoma kuongoza kwa malalamiko.

Pia amesema kuanzia mwezi huu wa Agosti ,2019 wanatarajia kufungua ofisi za TAKUKURU Eneo la Chemba huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano na Taasisi hiyo na kuweza kuitumia namba ya bure 113 pindi wanapoona vitendo vya rushwa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2YL6gTn
via

Post a Comment

0 Comments