DOWNLOAD APP YETU HAPA

NIMR YATOA MSAADA MUHIMBILI KWA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO WA MAFUTA

  Masama Blog      
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imetoa msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya Moto wa mafuta iliyotokea Agasti 9 mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa wameguswa kama taasisi na kuona umuhimu wa kutoa vifaa tiba kwa ajili ya majeruhi hao,

Amesema kuwa wadau wadau wameguswa na janga hilo na kuona umuhimu wa kusaidia vifaa tiba kwa ajili ya wagonjwa kwa wana mahitaji ya ziada katika kuokoa maisha yao.

“Tumetoa msaada kama taasisi katika kuhakikisha tunashiriki kwa pamoja katika kuwasaidia majeruhi waliobaki hospitalini kuweza kupona na kuendelea na majukumu yao ya uzalishaji mali” amesema Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Profesa Mgaya.

Katika hatua nyingine Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Watu Wenye Ulamavu Jenista Mhagama alitembelea Hospitali ya Taifa kuangalia huduma inayotolewa majeruhi wa ajali ya Moto wa mafuta iliyotokea Agasti 9 mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Yunus Mgaya akimkabidhi msaada wa vifaa tiba Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto wa mafuta uliotekea Agasti 9 mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Koleta Njelekela akikabidhi shemu ya msaada wa Sprite kwa Afisa wa Mapokezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Watu Wenye Ulamavu Jenista Mhagama (katikati) akizungumza wakati alipotembelea wodi ya majeruhi wa ajali ya moto wa mafuta uliotekea Agasti 9 mkoani Morogoro. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Yunus Mgaya watatu kutoka kushoto ni Dkt. Elisha Osati.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Yunus Mgaya akisalimiana na Daktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Elisha Osati wakati walipkwenda kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto wa mafuta uliotekea Agasti 9 mkoani Morogoro
Watendaji wa NIMR wakiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru 
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Yunus Mgaya akisaini kitabu cha Wageni Katika Ofisi ya Mkuruenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru wakati alipokwenda kutoa msaada.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Watu Wenye Ulamavu Jenista Mhagama akisaini kitabu cha Wageni Katika Ofisi ya Mkuruenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru wakati alipokwenda kuangalia hali za majeruhi wa ajali ya moto wa mafuta uliotekea Agasti 9 mkoani Morogoro.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2N5JoqW
via
logoblog

Thanks for reading NIMR YATOA MSAADA MUHIMBILI KWA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO WA MAFUTA

Previous
« Prev Post