Ticker

10/recent/ticker-posts

NGOs 158 ZAONDOLEWA KWENYE REJISTA YA MSAJILI


Mkurugenzi Msaidizi Usajili Bw. Baraka Leonard (kulia) akikabidhi cheti cha usajili kwa mmoja wa wadau waliofika kukamilisha usajili wakati wa zoezi la usajili wa mashirika hayo lilohitimishwa mwishoni mwa wiki kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. 
Mdau wa NGO Bi. Joanitha Mtayobya mkazi wa jijini Mbeya akipokea cheti cha usajili wa Shirika lake kutoka kwa Maafisa Wasajili wa Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati zoezi usajili wa mashirika hayo lilohitimishwa mwishoni mwa wiki kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. 
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi Vickness Mayao (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Msaidizi Uratibu na Ufuatiliaji Bi. Grace Mbwilo (katikati) na Bw. Baraka Leornard Mkurugenzi Msaidizi Usajili wakimsikiliza mdau wa NGO aliyefika kupata maelekezo kuhusu uhuishaji wa usajili wa Shirika lake wakati wa zoezi la kusajili NGOs lililohitimishwa mwishoni mwa wiki katika Nyanda za Juu Kusini Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. 
Timu wa wataalam wa usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya- Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii wakihudumia wadau waliofika kuhuisha usajili wao zoezi la usajili wa mashirika hayo lilolofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. 
Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Sekretatieti ya Mkoa wa Mbeya wakitoa ushauri wa kwa wadau waliofika kuhuisha usajili wa mashirika yao wakati wa zoezi la usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserika lilililohitimishwa katika Mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW 



Na Mwandishi Wetu Mbeya 

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini (NGOs) Bi. Vickness Mayao ameyaondoa Mashirika zaidi ya 158 kwenye Rejista ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. 

Hayo yamesema jijini Mbeya na Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa NGOs kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Grace Mbwilo kwa niaba ya Mkurugenzi na Msajili wa NGOs nchini. 

Bi. Grace amesema kuwa katika Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya Mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa Mabadiliko na Sheria Namba 3 ya Mwaka 2019, imefafanua bayana kuwa jukumu la kusajili mashirika yanayoendesha shughuli za kijamii, kiutamaduni, kiuchumi, utawala bora, haki za kibinadamu na mazingira katika ngazi ya jamii kwa lengo la kutogawana faida na ambazo hazina mrengo wa wa kukuza biashara, zimeelekezwa kusajililiwa na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs). 

“Mashirika yaliyoondolewa kwenye daftari la Msajili wa NGOs ni yale ambayo yalisajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 ambayo yanafanya kazi kwa lengo la kunufaisha wanachama wake, kugawana faida, yenye mlengo wa dini, yenye lengo la kukuza biashara na Bodi za wadhamini”, alisema Bi. Grace. 

Bi. Grace ameongeza kuwa, hatua ya kuyaondoa mashirika haya kwenye daftari la msajili wa NGOs imefikiwa kwa mujibu wa Sheria ya Marekebisho Na. 3 ya mwaka 2019 iliyoanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 Julai 2019. Kwa mujibu wa Sheria, Mashirika hayo yanatakiwa kwenda kujisajili chini ya Sheria husika ikiwemo Sheria ya Jumuiya za Kijamii(Sura ya 337), Sheria ya Munganisho wa Wadhamini(Sura ya 318) na Sheria ya Makampuni (Sura ya 212), na kwamba inatakiwa kukamilisha zoezi hili kabla ya tarehe 01 Septemba,2019. 

Ameeleza kuwa wa kuzingatia ufafanuzi wa mipaka ya usajili ulioainishwa na Sheria Namba 3 ya Mwaka 2019, Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) anayakumbusha Mashirika yanaofanya shughuli kwa lengo la kugawana faida, yenye mrengo wa dini na ambayo yana malengo wa kukuza biashara, kwamba mashirika ya aina hiyo yatafutwa kwenye daftari la Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali baada ya kipindi cha miezi miwili kuanzia tarehe 01.07.2019 na yatahamishiwa chini ya Mamlaka nyingine za Usajili kutokana na kukosa sifakuwa NGO. 

Katika kuhitimisha zoezi la usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali liliofanyika Mkoani Mbeya, Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali imewaagiza wadau wa mashirika yote yaliyosajiliwa kwa lengo la kuzalisha faida na kugawana faida kuhakikisha kuwa wanahamisha usajili ili kuhuisha taarifa zao kwa Msajili stahiki. 

Hatua hii imechukuliwa na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika hatua ya mwisho ya Usajili wa Mashirika hayo kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayohitimishwa mwisho wiki katika ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya na orodha ya Mashirika 158 yaliyoondolewa kwenye daftari inapatikana katika tovuti ya Wizara www.mcdgc.go.tzna ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. www.tnnc.go.tz


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/31Lq06r
via

Post a Comment

0 Comments