Ticker

10/recent/ticker-posts

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA, MWIGULU NCHEMBA AMEJIUZULU WADHIFA HUO

Aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara, Mwigulu Nchemba amejiuzulu wadhifa huo.
 
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo  jana Jioni katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mjini Dodoma

Akithibitha tukio hilo, Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi, Naoe Nnauye amesema, Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi utakaofanyika Octoba Mwaka huu

"Mwigulu alishamwambia nia hiyo Mwenyekiti wa Chama  Rais Jakaya Kikwete, nae Rais akamkubalia, na sasa  katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete amemkubalia Mbele ya wajumbe wa NEC".amesema Nape

Nape amesema kufuatia uamuzi wa mwigulu  kujiuzulu, Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete amemteua Msaidizi wake wa maswala ya siasa,Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC na Wakati huohuo kamteua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara Kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu Nchemba


from CCM Blog https://ift.tt/2YRYE0X
via

Post a Comment

0 Comments