Ticker

10/recent/ticker-posts

MWENYEKITI MPYA KAMATI BARAZA LA MAWAZIRI SADC PROFESA KABUDI ATAJA VITAKAVYOPEWA KIPAUMBELE

Na Said Mwishehe,Michuzi Blog

MWENYEKITI mpya wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)Profesa Palamagamba Kabudi amesema kwamba nchi za Jumuiya hiyo zinapasaa kutumia sekta ya viwanda katika kuleta maendeleo na kuondoa umasikini.

Profesa Kabudi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,.ameyasema hayo leo Agosti 13,2019 baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo ya uenyekiti wa kamati ya baraza la mawaziri kwa nchi SADC . Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Netumbo Ndaitwah ambaye ni Naibu Waziri Mkuu wa Namibia.

Hivyo baada Waziri Kabudi kukabidhiwa nafasi hiyo pamoja na mambo mengine amesema nchi za SADC zinapaswa kufikia maendeleo kwa kasi, hivyo sekta ya viwanda ni njia muhimu kufikia lengo hilo na kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake atakikisha sekta ya viwanda inapaswa kipaumbele.

"Nitahakikisha nashirikiana na wenzangu katika kamati na viongozi wa nchi kuchochea uanzishwaji wa viwanda kwa nchi wanachama kwani viwanda ndio chachu ya uchumi na maendeleo," almesema na Kuongeza anaamini iwapo kila nchi mwanachama itajikita kwenye uanzishaji wa viwanda na ujenzi wa miundombinu changamoto ya kiuchumi, ajira na huduma za jamii.

Aidha, amesema katika uongozi wao watapigania lugha ya kiswahili kutumika kama lugha rasmi ya SADC kwani Tanzania ina mchango mkubwa kwa jumuiya hiyo."Pia tutasimamia haki za watoto, wanawake na jamii kwa ujumla kwani hatutaki kumuacha mtu nyuma ndani ya jumuiya," amesema.

Wakati huo huowa upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Ndaitwah amesema nchi wanachama ili zinufaike na SADC ni lazima zisimamie utekelezwaji wa Eneo Huru la Biashara (FRA).

Aidha amesema pia mkakati wa kiendeleza wajasiriamali na vijana ni njia muafaka ya kuchochea maendeleo ya wananchi wa nchi za SADC.Pia amesema katika mwaka mmoja wa Uenyekiti wake umekuwa wa mafanikio kwa kupata ushirikiano wa nchi zote hivyo kuwaomba wajumbe wenzake waendeleze ushirikiano kwa mwenyekiti mpya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa SADC, Dk. Stergomena Tax amesisitiza kuwa ili jumuiya iweze kuwa na tija ni lazima vijana washirikishwe kwenye maamuzi kwa kuwa ni nguzo muhimu ya uchumi na maendeleo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2H0zanK
via

Post a Comment

0 Comments