Ticker

10/recent/ticker-posts

MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI AIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUJENGA RELI YA KISASA KWA FEDHA ZAKE ZA NDANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe amefanya ziara fupi kuona Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 22, 2019.

Katika ziara hiyo Bi. Anne alipata fursa ya kutembelea Stesheni ya reli ya kisasa inayojengwa eneo la Stesheni jijini Dar es salaam pamoja na kutembelea eneo la Vingunguti kuona kipande cha reli ya kisasa kilichotandikwa eneo hilo ambapo Bi Anne alionesha kufurashishwa na kasi ya ujenzi.

“Nimekuja kuona hatua kubwa ambayo serikali imechukua ya kujenga reli ya kisasa ninachoweza kusema kwa niaba ya nchi ninazoziwakilisha ni kwamba huu si mradi wa Tanzania pekee bali ni mradi wenye manufaa kwa nchi zilizofungamana katika ukanda huu” alisema Bi. Anne

Aidha Bi. Anne ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kwa kutumia mapato ya ndani pia ameahidi kuwa Balozi kueleza yale aliyoyaona katika Mradi wa SGR

“Naipongeza serikali ya Tanzania kwa kuamua kujenga mradi huu kwa kutumia vyanzo vya ndani" Nitafikisha ujumbe huu juu ya hiki tulichokiona leo” alisema Bi. Anne 

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa taasisi za kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia zinaweza kukamilisha Mradi huu kwa kuufadhili siku zijazo 
“Ni matumaini yangu kwamba kwa siku zijazo tutakapokuwa tunatafuta njia za kufadhili mradi huu taasisi za kimataifa ikiwemo benki ya dunia tutaweza kuja kukamilisha mradi huu” alisema Bi. Anne 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi na Miundombinu ya Reli Mhandisi Felix Nlalio amesema kuwa wameupokea ujio huo kwa furaha na kwa kuwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia amejionea mwenyewe kasi ya ujenzi na amefurahishwa na ubora wa wa kazi. 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ZbOOYz
via

Post a Comment

0 Comments