Ticker

10/recent/ticker-posts

MABALOZI 42 KUTEMBELEA MRADI WA UFUAJI UMEME RUFIJI

* Nchi zote za jumuiya SADC kushiriki mkutano huo wa kihistoria

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MABALOZI 42 wanaoiwakilisha nchi katika mataifa mbalimbali kesho Agosti 14 watatembelea mradi wa ufuaji umeme wa Julius Nyerere Hydro power Project (JNHPP) uliopo Rufiji Mkoani Pwani ili kuweza kujionea mradi hu unaotekelezwa na serikali ili kuweza kufanya diplomasia ya kiuchumi katika mataifa wanayotuwakilisha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Msemaji mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amesema kuwa mabalozi hao wameitwa rasmi kushiriki mikutano ya SADC inayoendelea ambapo wanatarajiwa kuwa wenyeviti wa SADC katika mataifa wanayoiwakilisha nchi kwa muda wa mwaka mmoja na wanaamini baada ya kutembelea miradi mbalimbali ukiwepo mradi mkubwa wa kufua umeme wa Julius Nyerere Hydro power wataenda kutumia vyema kofia zao za ubalozi katika kutangaza vyema diplomasia ya uchumi wa Tanzania katika mataifa mengine hasa yale wanayotuwakilisha.

Dkt. Abbasi amesema kuwa baada ya Profesa. Palamagamba Kabudi kupokea uenyekiti wa baraza la mawaziri wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa muda wa mwaka mmoja, kesho Agosti 14, Rais wa kwanza wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini atawasili nchini kwa matukio makubwa mawili.

"Rais Ramaphosa atawasili nchini kesho jioni kwa matukio makubwa mawili kwanza atakuwa na ziara ya kitaifa kwa siku tatu ambapo pia atatembelea kituo cha wapigania uhuru kilichopo Mazimbu Mkoani Morogoro, baada ya kumaliza ziara hiyo tarehe 16 Rais Ramaphosa ataungana na wakuu wa nchi na Serikali katika mkutano mkuu utakaofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu" ameeleza Dkt. Abbasi

Aidha amesema kuwa Agosti 15 mwaka huu Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ataongoza mhadhara wa wazi ambapo ataeleza uzoefu wake juu ya jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kueleza kuwa mhadhara huo ni wa wazi kabisa na kila mmoja anaweza kushiriki ili kuweza kupata uzoefu kutoka kwa mzee Mkapa.

Mkutano huo wa wakuu wa nchi, viongozi wa serikali na wafalme unatarajiwa kuhitimishwa rasmi tarehe 17 na 18 mwaka huu ambapo nchi zote wanachama zimethibitisha kushiriki mkutano huo na wawakilishi wa nchi hizo walianza kushiriki mikutano ya ndani na ile ya wiki ya nne ya viwanda ya SADC.
Msemaji mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akizungumza leo na Waandishi wa habari za mkutano wa SADC,katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijin Dar es Salaam,kuhusu uwepo wa Mabalozi 42 wanaoiwakilisha nchi katika mataifa mbalimbali kesho Agosti 14 watatembelea mradi wa ufuaji umeme wa Julius Nyerere Hydro power Project (JNHPP) uliopo Rufiji Mkoani Pwani, ili kujionea mradi huo unaotekelezwa na serikali ili kuweza kufanya diplomasia ya kiuchumi katika mataifa wanayotuwakilisha. Dkt. Abbasi amesema kuwa mabalozi hao wameitwa rasmi kushiriki mikutano ya SADC inayoendelea ambapo wanatarajiwa kuwa wenyeviti wa SADC katika mataifa wanayoiwakilisha nchi kwa muda wa mwaka mmoja

 Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa ukumbini humo.Picha na Michuzi JR.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2yXvn6q
via

Post a Comment

0 Comments