HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA LAVUKA LENGO, LAKUSANYA MAPATO KWA ASILIMIA ZAIDI YA 100%

  Masama Blog      
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha imevuka lengo la kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 105%,ambapo limekusanya jumla ya shilingi bilioni 16.4 lengo lilikuwa ni shilingi bilioni 15.6

Hayo yameelezwa na mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ,Kalisti Lazaro alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuelezea pongezi zilizotolewa na waziri wa Tamisemi Suleiman jafo kufuatia Jiji la Arusha kuongoza kwa makusanyo kwa mwaka 2018/19 katika majiji yote Nchini.

Amesema haijawahi kutokea Jiji la Arusha likaongoza kwa mapato ya ndani na hivyo wameweka mkakati ambalo utaliwezesha Jiji hilo kuendelea kuongoza kutokana na ubunifu wa kuongeza vyanzo vingine vya mapato na kuimarisha usimamizi wake.

Amesema katika kuhakikisha wanaimarisha ukusamyaji wa mapato ya ndani halmashauri hiyo ya Jiji imekabidhi vyanzo 14 vya mapato kwa Suma JKT ikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato yanayotokana na maliasili na machimbo ya Moramu kutokana na uadilifu wao.

Amesema kuwa halmashauri itaendelea kubuni vyanzo vingine vya mapato ikiwemo ujenzi wa maduka eneo la Ranger safari,kuboresha machinjio,kumaliza mgogoro wa Happy sausage.

Amesema kutokana na makusanyo hayo halmashauri imeweza kuondoa msongamano wa wanafunzi madarasani.utengenezaji wa madawati kwa kutumia karakana ya halmashauri hiyo ,wamekarabati kituo cha afya cha Moshono.

Amesema kuwa mwaka huu halmashauri inajenga shule za ghorofa kwenye shule za Moivaro,Muriet na Terati kupitia fedha za ndani.Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha Dakta Maulid Madeni amesema kuwa halmashauri imejipanga kukusanya shilingi bilioni 20 kwa mwaka 2019/20.

Amesema ukusanyaji huo utaiwezesha halmashauri hiyo kujitegemea kimapato ikiwemo kulipa mishahara ya watumishi wote na hivyo kuipunguzia serikali mzigo wa kutoa ruzuku kwa halmashauri hiyo.

Katika hatua ningine Mkurugenzi huyo amewaonya wafanyabiashara wakubwa wa maduka wanaotumia vitambulisho vya machinga kuendesha biashara zao,kwa kudao kuwa atawachukulia hatua kali kwa kuwa wanaikosesha halmashauri mapato .
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ,Kalisti Lazaro akiongea na waandishi wa habari.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2N6mf7x
via
logoblog

Thanks for reading HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA LAVUKA LENGO, LAKUSANYA MAPATO KWA ASILIMIA ZAIDI YA 100%

Previous
« Prev Post