Ticker

10/recent/ticker-posts

DKT. CHAULA AIPONGEZA TIMU YA WATOA HUDUMA ZA DHARURA SADC

Na Catherine Sungura,WAMJW

Katibu Mkuu,Wizara ya Afya Dkt.Zainabu Chaula amewapongeza timu ya wizara ya afya , taasisi zake pamoja na manispaa ambao walishiriki kutoa huduma kwenye mkutano wa 39 wa SADC ulomalizika leo jijini Dar es Salaam.

Dkt.Chaula ametoa pongezi hizo baada ya kumalizika kwa mkutano huo na kukutana na timu hiyo na kufanya mazungumzo na watumishi hao."Mmefanya kazi kubwa na nzuri sana katika utoaji huduma kwenye mkutano huu hakika mnastahili pongezi".Alisema Dkt.Chaula.

Aidha, Katibu Mkuu huyo alisema kama mtendaji mkuu atatafuta namna ya kuwawezesha watoa huduma wengine kujengewa uwezo na timu hiyo mahali walipotoka ili kutembea pamoja katika kutekeleza mikakati ya sekta ya afya katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania kwani wamepata ujuzi wa kutoa huduma hususani za dharura .

Timu hiyo ya kutoa huduma za dharura iliwajumlisha wataalam mbalimbali kutoka wizara ya afya,hospitali ya Taifa Muhimbili,Taasisi ya Mifupa(MOI), Taasisi ya Moyo(JKCI) pamoja na wataalam wengine kutoka hospitali za Manispaa za Ubungo,Ilala,Kigamboni,Kinondoni naTemeke



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2TLZB5Y
via

Post a Comment

0 Comments