Ticker

10/recent/ticker-posts

Anayedaiwa kumchoma mkewe moto kwa magunia mawili ya mkaa atishia waandishi wa habari

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV,

MFANYABIASHRA Khamis Luwonga maarufu kwa jina la Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, Naomi Marijani ametoa vitisho kwa waandishi wa habari wanaompiga picha akiwa mahakamani kuwa atawafanyia kitu kibaya ambacho mahakama haijakitarajia.

Mshtakiwa Said amedai hayo leo Agosti 13,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai mbele ya Hakimu Mkazi Salim Ally kwamba kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Baada ya kueleza hayo, mshitakiwa Said alinyoosha kidole na kuomba kuongea akasema, "Mheshimiwa nina kitu ambacho nataka nikueleze kuhusu Waandishi wa Habari, wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya mahakama sasa nakueleza hivi nitakuja kuishangaza mahakama nitafanya kitu kibaya sana;

"Kuna kesi ambayo inanikabili na sielewi hatima ya kesi yangu, hapa nilipo kichwa changu kimevurugika nina mawazo ya mtoto wangu na ninapofika hapa ili akili yangu itulie wanakuja kunipiga picha sasa nawaeleza kuwa nitafanya kitu kibaya ambacho mahakama haitatarajia,"

Kufuatia kauli hiyo ya vitisho kwa waandishi wa habari, Wakili Wankyo alimueleza mshitakiwa kuwa, kupigwa picha ni hali ya kawaida kwa mshitakiwa yeyote anayedikishwa mahakamani, wote wanapigwa picha, hivyo amemtaka awape uhuru Waandishi wa habari wafanye kazi yao.

"Lengo la Waandishi wa habari ni kutoa habari na kuwahabarisha jamii, hivyo kumbuka hii ni mahakama na hatujui kitu unachotaka kufanya ni kitu gani,"

Hata hivyo, Hakimu Ally anayeendesha shauri hilo, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Katika kesi hiyo, mshtakiwa anatuhumiwa kwa kosa moja la mauaji Kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura 16 kama kilochofanyiwa marejeo mwaka 2002

Katika kesi hiyo ya muaji namba 4 ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu, mshtakiwa Meshack alisambaza tangazo magazetini na kwenye mitandao ya Kijamii kuwa anamtafuta mke wake ambae alitoweka ghafla lakini baadae jeshi la polisi kupitia Mkuu wa Upepelezi wa kanda hiyo, Camillius Wambura alitangaza kumshikilia Luwonga akidaiwa kumuua na kisha aliuchoma moto mwili wa mkewe.
MFANYABIASHRA Khamis Luwonga maarufu kwa jina la Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, Naomi Marijani akifikishwa mahakamani.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2YLMzuZ
via

Post a Comment

0 Comments