Ticker

10/recent/ticker-posts

Waganga wa Kienyeji 65 Mbaroni Wakihusishwa na Mauaji ya Watoto

Polisi inawashikilia Waganga wa Kienyeji 45 kutoka Mkoani Simiyu na 20 kutoka Mkoani Njombe waliotiliwa shaka katika operesheni inayoendelea ya kuwasaka waliohusika na mauaji ya watoto

Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Simon Sirro amesema "Kuna Waganga ambao si wahalifu, lakini kuna wale Waganga ambao ni wahalifu hao tunadili nao moja kwa moja na tayari tumeshakamata Waganga 65"

Aidha, ameeleza sababu za kuwapo kwa matukio ya mauaji kuwa ni ramli chonganishi, ugomvi wa familia na wivu wa mapenzi na hivyo operesheni hiyo inaendelea kupita kwa kila Mganga ili kuwakagua

Mwezi Januari mwaka huu, kuliripotiwa matukio ya utekaji na mauaji dhidi ya watoto mkoani Njombe, huku wanaotekeleza ukatili huo wakidaiwa kunyofoa baadhi ya viungo kwenye miili ya watoto wanaowaua



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2NFQdO3
via

Post a Comment

0 Comments