Ticker

10/recent/ticker-posts

Je ni kweli kuwa Mwanamke Kupigwa Ndio Utamu wa Mapenzi?Soma hapa


Nimeliona sana hili. Wanakuja wanalia, ukiwauliza kwa nini. Boyfreind wangu kanipiga, siku nyingine tena hivyo hivyo. Huwa najiuliza kwa nini huwa wanaendelea na mahusiano. Nyinyi wadada kwa nini mnaendelea kwenye mahusiano ambayo kupata vipigo ni sehemu ya kawaida kwenu.

Naombeni uzoefu kidogo, jana usiku nilikuwa kwenye kituo Fulani cha Polisi hapa Dar. Jamaa alimdunda mpenzi wake ikambidi yule dada akodi pikipiki akimbilie polisi, jamaa yake pia akawa amekodi pikipiki kumkimbiza. Yule dada anakaribia kufika polisi jamaa yake akawa amemuwahi kwa mbele. Dada akawa analia huku akiwa analalamika amepigwa sana na mpenzi wake huyo. Polisi wakamweka jamaa ndani. Leo asubuhi nimefika pale kituoni kwa mambo yangu, nikamkuta yule dada kadamka mapema yupo pale polisi anamuombea msamaha mpenzi wake atoke. Kama mjuavyo, Polisi kuingia bure kutoka kwa rupia. Mdada kawapooza mandata, jamaa katoka wakaondoka.

Kitu ambacho ningependa kufahamu, je kuna aina ya mapenzi bila kipigo ayaendi? je wadada kitendo cha kupigwa ni ufahari? je kipigo wanachokipata ndicho uwafanya kushidwa kusema hapana?
Any contribution and experience are welcome