Ticker

10/recent/ticker-posts

Barcelona wamekataa ombi la Cristiano RonaldoUsiku wa December 16 2017 club ya Real Madrid ya Hispania ilifanikiwa kutwaa taji la pili mfululizo la club Bingwa Dunia kwa kuifunga Gremio katika mchezo wa fainali kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Ronaldo kwa faulo.
Staa wa soka wa Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kuelekea mchezo wao wa El Clasico dhidi ya FC Barcelona watakaoucheza siku ya Jumamosi December 23 2017, amewataka wachezaji wa FC Barcelona kuwawekea Real Madrid Guard of Honour wakati wanaingia uwanjani kutokana na Real Madrid kuwa mabingwa wa Ulaya na wametwaa taji la Club Bingwa Dunia.
“Itakuwa vizuri na ningependa kuona Barcelona wanatuwekea guard of honour kwa heshima ya kuwa mabingwa”>>>Ronaldo
Muda mchachee baada ya taarifa hizo kutoka mkurugenzi wa Barcelona Guillermo Amor amethibitisha kuwa Barcelona hawatowawekea Real Madrid a guard of honour kwa sababu hiyo sio sharia pili inatokea endapo Barcelona angekuwa kashiriki Ubingwa wa Dunia na yeye.