Ticker

10/recent/ticker-posts

BREAKING NEWZZZ…RC Makonda ataja wasanii wanaotumia dawa za kulevya..Wapo mastaa Wema Sepetu na wengine

Leo February 2, 2017 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa taarifa ya uchunguzi wake kuhusu biashara ya dawa za kulevya kwenye jiji la Dar es salaam na kuwataja Askari Polisi 9 wanaotuhumiwa kuhusika au kujihusisha na wafanyabiashara wa dawa hizo.
RC Makonda amezitaka mamlaka za kijeshi kuwaweka chini ya ulinzi askari hao kwa mamlaka yake ili waweze kutoa taarifa kwanini dawa za kulevya bado zinaendelea kuwepo.
Ameyataja baadhi ya maeneo ambayo Wamiliki wake wamepewa vibali vya kufanya 
biashara lakini wanatumia maeneo hayo kinyume na masharti ya biashara kwa kuuza 
dawa ya kulevya ambapo amewataka kufika kituo kikuu cha polisi kesho saa tano na wasipofanya hivyo atawafata mwenyewe.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ametaja orodha ya watu mbalimbali wanaojihusisha na dawa za kulevya jijini Dar es Salaam na kusema kuwa yupo tayari kwa ajili ya mapambano dhidi yao.
RC Makonda alisema kuwa yupo tayari kuuupoteza ukuu wake wa mkoa na hata kupoteza uhai wake lakini akifika mbele za Mungu apate kitu cha kusema kuwa alipewa nafasi na akatumia kupambana na janga hili linalohatarisha nguvu kazi ya taifa.
Katika orodha iliyotolewa na RC Makonda, wamo watu wa makundi mbalimbali ambapo kuna wanaouza dawa za kulevya, wanaosambaza na wanaotumia dawa hizo.
Katika watu hao kuna wasanii wa muziki nchini Tanzania, watu maarufu na maafisa wa Jeshi la Polisi ambao wamedaiwa kuwa wanakwamisha upelelezi juu ya kesi hizi
Miongoni mwa wanii waliotuhumiwa kutumia dawa za kulevya ni pamoja na Wema Sepetu, Rachel, Babu wa Kitaa, Mr. Blue, Chid Benz na wengine. Hapa chini ni video ya RC Makonda akizungumza na waandishi wa habari mapema leo;
WhatsApp Image 2017-02-02 at 1.07.35 PMWhatsApp Image 2017-02-02 at 1.07.35 PM (1)