
Kisoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Mafinga, amesema anafahamu kusoma na kwamba, tuhuma dhidi yake zimetokana na msimamo wake wa kusimamia rasilimali za kata yake na halmashauri.
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Mkoga alitangaza kumsimamisha diwani huyo wa Chadema kufanya shughuli za udiwani ikiwamo kuhudhuria vikao hadi suala lake litakapopatiwa ufumbuzi na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.