Ticker

10/recent/ticker-posts

WAYNE ROONEY AONGOZA MASTAA WA SOKA KUHUDHURIA NDOA YA TOM CLEVERLEY

  Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester United, Cleverley mchana wa leo alifunga pingu za maisha na mchumba wake wa muda mrefu Georgina Dorsett katika shughuli ya kifahari iliyofanyika huko Claridge.

  Ndoa hiyo ilihudhuriwa na mastaa wengi wa soka akiwemo nahodha wa klabu ya Manchester United na England Wayne Rooney ambaye pia aliongozana na mkewe Coleen, Chris Smalling wa Man United, Danny Welbeck na wachezaji wengine, pia alikuwepo muimbaji wa band ya The Saturdays, Rochelle Humes. 
Cleverley na Mkewe wakiwa wanatoka kanisani

   
Mchezaji wa Arsenal – Danny Welbeck
Wayne na Coleen Rooney Harusini
Wanandoa kwenye pozi la picha