Ticker

10/recent/ticker-posts

MAHAKAMA YA AFRIKA KUHAMASISHA WADAU NCHINI DJIBOUTI

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye makao yake makuu jijini Arusha itafanya ziara ya kikazi nchini Djibouti ili kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kwa lengo la kuiitangaza Mahakama hiyo ya Umoja wa Afrika (AU). 

Ujumbe wa ziara hiyo inayoanza Mei 21 hadi Mei 24 pia unatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Djibouti, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Sheria na Spika wa Bunge . 

Rais wa Mahakama ya Afrika, Mheshimiwa Jaji Sylvain Ore’, alisema wakati wa ziara hiyo itaendeshwa semina inayolenga kukuza uelewa wa wadau hao juu ya uwepo wa Mahakama na jinsi inavyoendesha shughuli zake ikiwemo kupokea mashauri. 

Kwa mujibu wa Jaji Ore’,Uelewa wa wadau hao kuhusu uwepo wa AfCHPR pia utaleta hamasa kwa nchi nyingi zaidi za AU kuridhia itifaki iliyoanzisha mahakama hiyo na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali mamlaka ya Mahakama hiyo kuweza kupokea kesi za watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGOs). 

“Ili Mahakama iweze kufanikisha malengo yake na pia kuimarisha mfumo wa Haki za Binadamu barani Afrika,nchi nyingi za Umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa mujibu wa kifungu cha 34(6)”,Alisisitiza Jaji Ore’. 

Tangu mwaka 2010,Mahakama hiyo ya Afrika imefanikiwa kuendesha programu mbalimbali zinazolenga kutoa elimu ya uwepo wa AfCHPR pamoja na shughuli zake katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Chad,Ethiopia,Afrika ya Kusini,Ghana,Malawi,Kenya,Uganda,Zambia,Morroco na Tunisia.Nchi nyingine ni IvoryCoast,Cape Verde,Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi,Misri na GuineaBissau. 

AfCHPR ilianzishwa mwaka 2006 na ilianza shughuli zake rasmi mwaka 2008.
 African Court in Arusha, Tanzania
Rais wa Mahakama ya Afrika, Mheshimiwa Jaji Sylvain Ore’,



from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2Qb1eIo
via

Post a Comment

0 Comments