Ticker

10/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO KWA MABALOZI WAPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha Mabalozi sita aliowateua jana kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali na kuwapa maagizo ya kuitangaza vema na kuiletea maendeleo Tanzania.

aHafla ya kuapishwa kwa Mabalozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza baada ya Mabalozi hao kula viapo vyao, Rais Magufuli amewataka kuiwakilisha vizuri Tanzania katika nchi walizopangiwa kwa kuhakikisha wanasimamia maslahi ya Tanzania.
“Nendeni mkatekeleze kazi zenu kwa upendo mkubwa mkijua umma wa Watanzania upo nyuma yenu, Maslahi ya Watanzania yakawe mbele, Tanzania kwanza ikawe mbele, na mimi nina uhakika mtakuwa mmewafanyia Watanzania mema na mazuri sana”
Rais Magufuli akizungumza na mabalozi baada ya kula viapo
“Ukiona kizuri chochote kwaajili ya Watanzania kilete, mkatetee Tanzania, mkajenge uchumi wa Tanzania, mkaimarishe mahusiano ya Tanzania, mkajenge urafiki wa Watanzania, mkajenge biashara za Watanzania” 
Mabalozi walioapishwa ni Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi -Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. James Alex Msekela - Baloziwa Tanzania Geneva - Umoja wa Mataifa, Mhe. Mbelwa Brighton Kairuki - Baloziwa Tanzania nchini China, Mhe. Fatma Mohamed Rajab - Baloziwa Tanzania nchini Qatar, Mhe. George Kahema Madafa - Balozi wa Tanzania nchini Italy, Mhe. Prof. Elizabeth Kiango Kiondo - Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.
Rais Magufuli akimuapisha Mhe. Prof. Elizabeth Kiango Kiondo - Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.
Wakati huo huo
Baada ya kula kiapo cha Uadilifu, Mhe.Jaji Mstaafu Harold Reginald Nsekela ameongoza kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kwa Mabalozi sita walioapishwa leo kwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.