Msanii na pia ni Meneja wa msanii mwenzake kutoka Kenya, Akothee. Jaguar ambae kwa sasa ameamua kujikita zaidi kwenye shughuli za kiserikali ili kusudi kuwasaidia wananchi wa Kenya.
Ni wiki sasa imepita baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa maji na Wizara ya Maji na Umwagiliaji Nchini Kenya, msanii Charles Njagua Maarufu kwa jina la Jaguar.
Jaguar amesema atafanya kampeni kuhakikisha kuwa wakazi wa vitongoji duni vyote nchini wanapata maji safi na Salama.
WhatsApp-Image-2016-11-30-at-00.20.19-295x300
Msanii Jaguar Akiwa na Wananchi huko Kibera nchini Kenya.
NACADA
Huku akiahidi kufanya kazi kiuadilifu kama Rais Magufuli, Tanzania.
“Nimeaminiwa kufanya kazi na wakenya wote hivyo nitafanya kazi kuhakikisha kila mkenya anakuwa na maji safi, nataka kuona tunasonga mbele, sitakuwa mbele yaani nitakuwa Magufuli nawaambia”
Msanii huyo alipewa wadhifa huo juma lililopita katika hafla iliyo hudhuriwa na watu maarufu, miongoni mwao Waziri wa Maji, Eugene Wamalwa na Makamu wa Rais Nchini Kenya William Ruto.

SHARE

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Top