Askofu Gwajima akutwa na kesi ya kujibu.......Mahakama Yamtaka Ajieleze Disemba 13Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemuona Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima anayekabiliwa na kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha, ana kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha alitoa uamuzi huo jana baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wa upande wa Jamhuri pamoja na vielelezo.

Alisema kutokana na ushahidi huo, ameona upande wa Jamhuri umejenga kesi hivyo Gwajima na wenzake watatu, wana haki ya kujitetea, kuita mashahidi au kukaa kimya.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa washtakiwa watajitetea kwa njia ya kiapo na watakuwa na mashahidi watatu.

Hakimu Mkeha alisema Desemba 13, mwaka huu, washtakiwa watajitetea na siku hiyo atasikiliza utetezi wa washtakiwa wote wanne pamoja na mashahidi wao.

Mbali na Gwajima, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni msaidizi wa askofu huyo, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mnzava (43) na mkazi wa Kimara Baruti, Geoffrey Milulu (31).

Inadaiwa kuwa, Machi 29 mwaka jana, katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A, washitakiwa walikutwa wakimiliki bastola aina ya Baretta yenye namba CAT 8802 bila kuwa na kibali kutoka mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

Aidha, inadaiwa washtakiwa hao walikuwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya shotgun. Gwajima anadaiwa kushindwa kuhifadhi silaha katika hali ya usalama.


Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top