Mara nyingi nilikuwa nikimtembelea rafiki yangu, halafu nilijisemesha  mwenyewe  kwa ajili ya kujifurahisha. Lakini pia nilikuwa na tumaini kwamba ataweza kuniondolea wasiwasi na kuniambia kitu ninachohitaji kusikia.
Topic ya kikao chetu? ilikuwa ni mapenzi, bila shaka , nilihitaji kujua ni lini nitakutana na mwenza nimpendae. Mwitikio wake ulikuwa, sio karibu! alinitazama, halafu anapigapiga tumbo langu na kusema, Utakapopunguza Uzito, utapata mtu umpendae, unahitaji kuwa na afya ya kumvutia unaemuhitaji.
Kujipenda Haitegemei Jinsi Unavyooneka, Inategemea Na Jinsi Unavyoishi.
Huyu mwanamke hakujua uwazi kuwa nimeweka maisha yangu kwenye ujumbe wa kujipenda mwenyewe na kutafuta mapenzi yangu mwenyewe. hakufahamu kuwa nimepigania miaka mitatu kupumua kwa kujihujumu, ugonjwa wa kutokula, na matatizo ya wembamba. hakufahamu kuwa nimekabiliana na huzuni na kupata mapenzi ya kweli yangu mwenyewe. furaha ya kujitambua Duniani.
Hakufahamu kuwa ni mwenye afya tele sasa kuliko kule mwanzo kwa sababu nakula vizuri, nafanya mazoezi kila siku, na kitu cha muhimu zaidi  najisemea mema mwenyewe na mimi ndio rafiki wa mimi peke yangu.
Huyu mwanamke aliniambia nisingeweza kupata ninachohitaji kwa sababu ya mwonekano wangu, kitu cha kusikitisha ni kwamba hakuwa peke yake, nilikuwa nikiamini hivyo. nilikuwa nikifikiria kama nina uzito wa kupunguza, hakuna mtu angenipenda. Lakini sasa, nafahamu , kujipenda haitegemei jinsi unavyoonekana, ni jinsi unavyoishi.
Tunahitaji kuacha kuamini mawazo ya watu wengine kuhusu kwa nini hatupati tunachohitaji.
Mimi sio Single eti kwa sababu ya jinsi ninavyooneka. Sote tuna mapungufu, na katika kutafuta mapenzi ya kudumu, mara nyingi tunaonekana kama kutafuta mtu sahihi. tunafikiria vitu kama , kama nikipoteza uzito , nitakutana na mtu wa maisha yangu. my soulmate. kama nywele zangu zingekuwa nzuri, miguu yangu ingekuwa imejazia, macho yangu yangekuwa makubwa, pua yangu ingekuwa ndefu, kiuno, hapo labda ndio ningepata ninachohitaji na ningekuwa na furaha..” tuache kujishusha wenyewe eti hatuko vizuri.
Upekee wako ni Zawadi yako, kwa hio furahia, heshimu ilo, utukuze.
Yapo mafunzo mengi hasa kwa wanawake kufundishwa kujipenda kwanza wenyewe, sasa nashangaa kwa nini mimi bado nipo single. lakini nilijikumbusha kuwa, lengo sio kubadilika kwa ajili ya kufit wengine, bali ni kujikubali wenyewe na kujipenda tulivyo. hiki ndicho kitu kinachosababisha mvuto wa mapenzi ya kweli kwetu.
Kuna vitu vinavyotufunga kutoka katika kitu tunachokitaka. kama unahitaji mapenzi ya kudumu na hayatokei, inaweza kuwa ni moja ya hizi sababu. lakini usihofu– utakabiliana nazo kwa furaha na kwa urahisi.
1.Kitu Wanachotaka Wengine Na Kutarajia Kupata Kwetu.
Watu wanaoamini kuwa wenye uzito mkubwa hawana afya na hawawezi kupata mtu wa kuwapenda. hizi ni Imani zao, sio zangu.na wala sio zako. Inawezekana una bibi yako anatamani kuona Unaolewa. misukumo hii inatufanya kujiona kuwa tumekwama mahali.
Acha kusikiliza hayo, na usitake kuwafurahisha watu. Una safari ya kipekee ya maisha yako. kwa hio heshimu hilo, mahali ulipo na usherehekee.Kumbuka ,jinsi unavyojisikia maisha yako ni zaidi ya jinsi ya mwonekano.
2.Faraja Zetu.
Wengi hutafuta mapenzi ya kudumu, lakini wakiwa wanafahamu kuwa wanahitaji faraja. unaweza ukawa unaishi maisha kwa njia nzuri;Una routines zako, mazingira na tabia ambazo unaweza kuwa unafahamu kuwa hauko tayari kuziacha.
Kitu kilichopo ni kwamba mtu huchoka kubaki peke yake na kuhitaji mtu wa kuwa nae. kila mtu ana tabia zake tangu akiwa anakua. huwezi kubadilisha ili mtu fulani akupende. Lakini unahitaji kuwa mkweli ili mtu akupate jinsi ulivyo. Tabia yako ya kawaida itakusaidia , kuliko kujifanyia tabia ambazo sio zako.
Hayo ni mapenzi ya kikomedi. hata ukifanya nini. kuwa makini kwenye uchaguzi na tabia, utaweza kumvutia mtu mwenye kukupenda ulivyo.
3.Tunachosema Kuhusu Sisi Wenyewe.
Kama unaongea na rafiki zako kwa njia unavyojisemea mwenyewe, unaweza kupata chochote? Ukweli ni kwamba, tunaweza kujianika mwenyewe. jinsi unavyojisemea wewe ndio njia ya kuvutia wengine, Kama unajishusha na kujidharau, itakuwa vigumu kuruhusu mapenzi ndani yako.
Badala ya kujilalamikia , geuza hilo liwe la kujipenda, jipongeze, na uone uzuri ndani mwako. your amazing, na hii ni yako peke kwenye sayari hii.upekee wako ni zawadi yako. kwa hio furahia, sherehekea na uheshimu.
4.Malengo Yetu Kwa Wengine.
Tunapotaka kitu,mara nyingi tunaviona kwa wengine, tunafikiri ” wale watu wanaonekana na furaha kubwa kwenye mahusiano yao.” halafu tunajisikia vibaya wenyewe kuwa single.
Malengo haya yametufanya tuwe wazi kwenye mapenzi ya kudumu. kila mara unapoona ndoa za furaha, rudisha utulivu wako kwenye uwezekano kuliko kile unachobahatika.
Ina maana kuwa badala ya kuhisi unyonge , rudia furaha ya kuwafurahia. ” Kuwa ulimwengu wako unakuonyesha kinachowezekana, kiko njiani kwa ajili yako”.
5.Ukosefu Wa Imani Yetu.
Kikwazo kikubwa cha wazi wa mapenzi ni Ukosefu wa Imani yetu katika mpango wa maisha. Tunahitaji kuamini katika maisha yetu ya baadae na kufahamu kuwa tunastahili kwenye nia zetu, na hili linatokea tunapoweka Imani kwa kile kisichojulikana.
Ukweli ni kwamba, Kuna muda wa Mungu kwa kila kitu katika maisha yetu. na tunapoamini mpangilio tutaepukana na mahangaiko ya kufikiria kwamba tumekwama.
Amini Mpango wa Mungu na uwe na utulivu wakati huu. Badala ya kuhangaika na kitu gani kinakosekana, kazania kinachoendelea vizuri. Anza kuishi maisha yako kwa malengo yaliopo sasa, na utajisikia Amani na urahisi.Acha kusikiliza Mawazo ya watu Wengine.