Wengine 10 wafuzu kujiunga Azam Fc AkademiVIJANA 10 wenye umri chini ya miaka 17, wamefanikiwa kuchaguliwa kwenye majaribio ya wazi yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, jana Jumamosi katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.        
         

Huo ni mwendelezo wa mpango wa mabingwa hao wa kutengeneza timu bora ya vijana wa umri huo kwa ajili ya kuwatumia kwa miaka ijayo na wengine kunufaika nao kwa kuwauza.

Katika majaribio hayo walijitokeza jumla ya vijana 406 kutoka sehemu tofauti na jiji hilo kabla ya kuchujwa na kufikia 29 na hatimaye kupatikana 10, ambao wataingia kwenye mchujo wa mwisho utakaofanyika Azam Complex mwezi ujao.

Mchujo huo wa mwisho utashirikisha vijana wengine 50, waliochaguliwa kwenye maeneo mengine saba nchini ambayo Azam FC tayari imeshayatembelea, ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro iliyojumuisha pia vijana wa mkoa wa jirani wa Dodoma pamoja na Visiwani Zanzibar (Unguja na Pemba).

Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg, anayeendesha zoezi hilo amefurahishwa na wingi wa vijana walijitokeza jijini Mbeya huku akiridhishwa na vipaji vyao akidai kuwa huo ni mwanga mzuri wa kutengeneza kikosi bora kwa manufaa ya Azam FC na Taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa ripoti ya mpango huo, mpaka sasa Azam FC imeshawafanyia usaili vijana 2,999 kwenye maeneo yote nane waliyotembelea, wakichaguliwa 60 pekee kwa ajili ya kuingia katika mchujo wa mwisho wa fainali utaotoa vijana bora watakaounda timu hiyo.


Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top