WCB YALAMBA DILI LA ZAIDI YA BIL 2 KUTOKA KAMPUNI YA KIMAREKANI YA UNIVERSAL | Masama Blog

WCB YALAMBA DILI LA ZAIDI YA BIL 2 KUTOKA KAMPUNI YA KIMAREKANI YA UNIVERSAL

Kupitia kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds FM Radio msanii Diamond Platnumz ameweza kufunguka mambo mengi sana yanayo husu label ya WCB.

Moja ya jambo aliloweka wazi ni kuhusu Dili walilolipata Label ya WCB ya kusimamiwa kazi zao za kimuziki na Kampuni kubwa ya Universal. kampuni hiyo itakuwa ikisambaza kazi za WCB kimataifa zaidi, Hii itakuwa ni fursa nzuri kwa Label hiyo kupenyeza muziki wa kibongo ki-International.

Katika Mkataba huo WCB imeweza kuingiza Dola za kimarekani Milioni Moja (karibia bilioni 2 fedha za kitanzania.).

Hebu msikilize hapa Diamond akifunguka mwenyewe katika hii Interview.

SHARE


Back To Top