VIDEO:Angalia Mabishano ya Mbowe na Naibu Spika Kuhusu Tuhuma za Wabunge wa CCM Kuhongwa Milioni 10 Kila Mmoja ili Wapitishe Muswada wa Habari | Masama Blog


VIDEO:Angalia Mabishano ya Mbowe na Naibu Spika Kuhusu Tuhuma za Wabunge wa CCM Kuhongwa Milioni 10 Kila Mmoja ili Wapitishe Muswada wa Habari


Mbowe alisema kuwa Wabunge wakiwemo Mawaziri walihongwa shilingi milioni 10 kila mmoja ili waweze kusaidia kupitisha Muswada wa Habari unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni kesho.
Lakini Naibu spika alikataa  Waziri mkuu kujibu swali la Mbowe kwa  madai kuwa swali hilo halihusu sera, huku Mbowe akidai linahusu sera kwa kuwa ni rushwa kwa wabunge
Wasikilize Hapo chini: 

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu leo asubuhi  alidai kuwa, mnamo siku ya Jumanne tarehe 25/10/2016 saa mbili usiku kiliitishwa kikao cha wabunge wa CCM ambacho Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa Mwenyekiti, na kilihudhuriwa na Katibu MKuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwa ajili ya kujadili Muswada wa Habari.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200