VIDEO: RC Makonda Alivyoamuru Wenyeviti Watano Kuchukuliwa na Polisi Katikati ya Mkutano | Masama Blog


VIDEO: RC Makonda Alivyoamuru Wenyeviti Watano Kuchukuliwa na Polisi Katikati ya Mkutano

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda November 28 2016 alimaliza ziara ya Dar Mpya ambayo alizunguka maeneo tofauti ya jiji la Dar es salaam kwa siku 10 kusikiliza na kutoa majibu ya kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Akiwa kwenye mkutano wa  mwisho Mwabepande suala kubwa lililojitokeza ni kuhusu utapeli wa viwanja, wananchi walilalamikia kutapeliwa viwanja wakati walivyouziwa kulikuwa na baraka zote kutoka kwa wenyeviti wa mtaa. Baada ya tuhuma hizo kutolewa wananchi waliwataja wenyeviti walioshiriki kuuza viwanja kitapeli na RC Makonda akaamuru wachukuliwe na polisi  kwa hatua zaidi. Unaweza kuangalia video hii hapa chini. 

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200