Lebo ya The Industry iliyo chini ya umiliki wa kundi la Navy Kenzo imeachia ngoma nyingine ya msanii wao Wildad iitwayo Get It On.

 

Msanii huyo wa RnB amekuja kuteka mioyo ya kina dada kwa muonekano na sauti yake ambayo ni kivutio kikubwa katika kuimba kwake.

Akizungumza mara baada ya kuachia wimbo huo kwenye ofisi za Mkito, Masaki jijini Dar Wildad amesema, “Nimekuja kuleta ladha mpya ya RnB na kipaji changu ni cha kipekee na lengo kubwa la ni kuvuka mipaka”.

Wildad alijiunga na “The Industry” May mwaka huu wa 2016 na ngoma yake pamoja na video vinaashiria kuwa ana matarajio makubwa ya kuifikisha RnB ya Tanzania kwenye matawi ya juu.

Itazame hapa video yake.

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Top