15056662_331170897262349_6840282975670632448_n
Baada ya Ommy Dimpoz kueleza kwa kina kuhusiana na sababu iliyopelekea wakakosana na Diamond, muimbaji huyo wa Salome, amejibu kupitia Instagram.

Majibu ya Diamond ni ya mafumbo kiasi na tayari yamepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki huku wengi wakichukizwa na kauli yake.
Ameandika:
Basi nlivyokuwa Mshamba Nikajua Mtu Mwenye Roho Mbaya na Mbinafsi Mungu ndio Humuadhibu na Kumfelisha kwa Roho Mbaya lake ili asifanikiwe… halaf Mwenye Roho nzuri Mungu Humlipa kwa Kumfanya afanikiwe zaidi na zaidi…. Asa nashangaa Mwenye Roho Mbaya eti Mungu ndio Kamfanikisha, halaf Maskini ya Mungu Mwenye roho nzuri eti Miguu juu…..au pengine labda Mwenyez Mungu kakosea kidogo kwenye Mahesabu yake..???😟 hii nayo ni #KOKORO ujue
Itazame hapo chini interview ya Ommy Dimpoz.

SHARE

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Top