Kuna mtoto aliibiwa mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka miwili.Mtoto huyo aliibiwa na bibi mmoja ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa kazi za nyumbani.
Siku aliyomuiba bibi alikuwa amepoke mshahara wake na alimuaga muajiri wake kuwa anaenda kununua kandambili huku akiwa amebeba mtoto mgongoni na ndio alitumia nafasi hiyo kutoroka na mtoto.
Jitihada za kumtafuta mtoto tangu kipindi hiko ziligonga mwamba mpaka mwaka huu ambapo mtoto huyo alionekana  na msamaria mwema ambaye alikuwa akiifahamu familia hiyo na kuwataarifu kuwa amemuona mtoto ambaye anahisi ni yule aliyeibiwa mwaka 2003.
Mtoto huyo ambaye kwa sasa ni binti mwenye umri wa miaka 18 ameoenaka jijini Mwanza na kwao kabsa ni  Sengerema na alikuwa akiishi na baba na mama yake wa hukohuko.Katika kuhojiwa iligundulika kuwa yule bibi aliyemuiba kipindi hiko yupo na mtoto anamfahamu kama bibi yake mzaa mama.
photogrid_14787728771751
Huyu ndiye mtoto ambaye inadaiwa aliibiwa mwaka 2003 akiwa na miaka miwili
  Polisi walifika hadi nyumbani kwa bibi na bibi alisisitiza kuwa huyo ni mjukuu wake na wazazi wa huko sengerema walidai pia kuwa huyo ni mtoto wao lakini vyeti vya uthibitisho  kuwa huyo ni mtoto wao viliungua na moto.
Mpaka sasa kesi ipo polisi na imeamuriwa wazazi wa pande zote mbili wapime DNA ili mtoto aweze kujulikana ni wa nani.Majibu ya DNA yatatoka baada ya wiki tatu

Msikilize MAMA ambaye mwanae alipotea mwaka 2003 akielezea jinsi ilivyokuwa na walipofikia
photogrid_14787693536171Kushoto ni mtoto alivyo sasa,kulia ni Mama anayedai huyo ni mtoto wake aliyeibiwa mwaka 2003 akiwa na miaka miwili
Mtoto  alipotea tarehe 9 mwezi wa tatu mwaka 2003,akiwa na miaka miwili,tulimtafuta sanaa hadi kwenye vyombo vya habari lakini hatukumpata,aliibiwa alikuwa kwa shangazi yake kulikuwa na mama alikuwa akifanya kazi za ndani akafanya kazi mwezi mmoja siku anayopewa mshahara wake ndipo alipoondoka na mtoto jioni mida ya magharibi akasema nanunua kandambili akatoka na mtoto ndio jumla jumla mpaka jumamosi ya juzi nikapigiwa simu na babayake mkubwa akaniambai kuna sehemu tumeitwa kuna mtoto tumeenda kumungalia binti tunavyomuona ni kama yule wa kwetu,tumeambiwa tuwezi kufwatilia kesi polisi mpaka mama yake pia awepo…
Audio Player
Ilibidi tuondoke na maaskari hadi sengerema,kiukweli nilivyomuona yule mtoto ni wa kwangu hadi hata nilivyomuona kwa mbali mpaka mwili ulinisisimuka,Tulivyofika tukarepoti polisi ikabidi maaskari na maafisa wa ustawi wa jamii waende hadi huko kijijini kwao kufika hawakuwakuta wazazi wake,ilibidi wawahoji majirani na balozi ambao walida kuwa wazazi wahuyo mtoto walihamia hapo kipindi mtoto huyo akiwa na miaka mitatu…
Audio Player
Mtoto alivyowaelezea maaskari kuwa alitoroka huko sengerema tangu mwezi wa nne kutokana na manyanyaso kutoka kwa Babayake anaambiwa akachunge shule haendi mara nyingine anaambiwa aende akamtafute babayake, ndipo akaamua kutoroka kwenda mwanza  kutafuta kazi na rafiki zake,ndipo akakutana na mtu kwenye basi ili wakifika huku wampigie mtu anayehitaji msichana wa kazi,baada ya namba kuwa haipatikani yule dada waliokutana nae kwenye basi alimchukua kwenda kukaa nae hapo Nyakato Mwanza,Sasa kilichotokea mama mwenye nyumba wa huyo dada ndio alimtambua akasema mbona huyu mtoto anafanana na familia ya yule mtoto aliyepotea mwaka fulani ndio akawaita ndugu wa babayake ili kufwatilia kila anayemuona akawa anasema ndio yeye basi ndio ikabidi wakatoe ripoti polisi…
Audio Player
kwanza zilitolewa picha za wazazi wa mtoto pamoja na bibi mzaa mama yake ndipo katika hizo picha tukamtambua yule bibi ambaye alikuja kufanya kazi,maaskari wakamtumia mtoto kwenda kwa bibi na walivyofika nyumbani kwa bibi hawakujitambulisha kama maaskari walijifanya kama wanataka kumposa mtoto wako,kwanza bibi alishtuka kumuona mtoto akasema umekuja mjukuu wangu,na pale kwa bibi tulikuta watoto wengi ambao pia bibi alidai ni watoto wake,Na wazazi wa mtoto walipoulizwa vielelezo vy kuwa mtoto ni wao walidai kuwa vimeungua na moto,bibi mpaka sasa hivi yupo chini ya ulinzi wa polisi
Audio Player

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100 
Top